9 Juni
Mandhari
(Elekezwa kutoka Juni 9)
Mei - Juni - Jul | ||||||
1 | 2 | 3 | 4 | 5 | 6 | 7 |
8 | 9 | 10 | 11 | 12 | 13 | 14 |
15 | 16 | 17 | 18 | 19 | 20 | 21 |
22 | 23 | 24 | 25 | 26 | 27 | 28 |
29 | 30 | |||||
Kalenda ya Gregori |
Tarehe 9 Juni ni siku ya 160 ya mwaka (ya 161 katika miaka mirefu). Mpaka uishe zinabaki siku 205.
Matukio
[hariri | hariri chanzo]- 1534 - Jacques Cartier, Mzungu wa kwanza kufikia mto Saint Lawrence
- 1815 - Mwisho wa Mkutano wa Vienna uliorekebisha hali ya siasa ya Ulaya
- 1856 - Wamormoni 500 wanatoka mji wa Iowa City katika jimbo la Iowa na kuelekea magharibi kwenda mji wa Salt Lake City katika jimbo la Utah wakibeba mali zao zote kwenye mikokoteni
Waliozaliwa
[hariri | hariri chanzo]- 1640 - Kaisari Leopold I wa Ujerumani
- 1672 - Tsar Peter I wa Urusi
- 1843 - Bertha von Suttner, mwandishi Mwaustria, na mshindi wa Tuzo ya Nobel ya Amani mwaka wa 1905
- 1875 - Henry Dale, mshindi wa Tuzo ya Nobel ya Tiba mwaka wa 1936
- 1935 - Pius Msekwa, mwanasiasa kutoka Tanzania
- 1940 - Abdisalam Issa Khatib, mbunge wa Tanzania
- 1963 - Johnny Depp, mwigizaji wa filamu kutoka Marekani
- 1988 - Flaviana Matata, mwanamitindo kutoka Tanzania
Waliofariki
[hariri | hariri chanzo]- 68 - Nero, Kaisari wa Dola la Roma, anajiua
- 373 - Mtakatifu Efrem wa Syria, mtawa, shemasi na mwalimu wa Kanisa huko Mesopotamia
- 597 - Mtakatifu Kolumba, mmonaki mmisionari nchini Uskoti
- 1597 - Mtakatifu Yosefu wa Anchieta, Mjesuiti mmisionari nchini Brazil
- 1870 - Charles Dickens, mwandishi Mwingereza
- 1959 - Adolf Windaus, mshindi wa Tuzo ya Nobel ya Kemia mwaka wa 1928
- 1974 - Miguel Asturias, mshindi wa Tuzo ya Nobel ya Fasihi mwaka wa 1967
- 1987 - Elijah Masinde, mwanzilishi wa Dini ya Musambwa
- 1989 - George Beadle, mshindi wa Tuzo ya Nobel ya Tiba mwaka wa 1958
- 2005 - Richard Eberhart, mshairi kutoka Marekani
- 2007 - Achieng Oneko, mwanasiasa wa Kenya
- 2022 - Matt Zimmerman, mwigizaji wa Canada
Sikukuu
[hariri | hariri chanzo]Wakristo wengi, wakifuata mapokeo ya Roma, huadhimisha kumbukumbu za watakatifu Efrem wa Syria, Primo na Felisiani, Diomede wa Nisea, Vinsenti wa Agen, Masimiano wa Siracusa, Kolumba, Richadi wa Andria, Yosefu wa Anchieta n.k.
Viungo vya nje
[hariri | hariri chanzo]Makala hii kuhusu mambo ya kihistoria bado ni mbegu. Je, unajua kitu kuhusu 9 Juni kama enzi zake au matokeo yake? Labda unaona habari katika Wikipedia ya Kiingereza au lugha nyingine zinazofaa kutafsiriwa? Basi unaweza kuisaidia Wikipedia kwa kuihariri na kuongeza habari. |