Nenda kwa yaliyomo

Mwanamitindo

Kutoka Wikipedia, kamusi elezo huru
Mwanamitindo Gisele Bündchen akitembea kwa mtindo wa en:catwalk.
Mwanamitindo akitembea kwa mtindo wa en:catwalk

Mwanamitindo ni mtu mwenye kazi ya mkao, au kuonesha kazi za sanaa au maonyesho ya mavazi, kwa kawaida hutafuta soko kwa ajili ya bidhaa. Mara kwa mara hutumiwa kwenye matangazo ya televisheni na vyombo vya habari vya uchapishaji, kwa mfano magazeti na majarida[1].

Aina za wanamitindo

[hariri | hariri chanzo]

Kuna aina chungumzima za wanamitindo. Baadhi yao hutumia sehemu fulani tu za miili yao. Kwa mfano, mwanamitindo wa mkono ni mtu ambaye hutumia mikono yake tu kufanyia shughuli za kiuanamitindo. Mwanamitindo wa mkono hutumika kuoneshea bidhaa fulani, kwa mfano pete au saa. Wanamitindo wa aina hii kawaida hutumiwa kwa ajili ya matangazo tu, basi. Msanii Marc Engelhard hufanya sehemu za mwili wake zipatikane kwa picha hiyo.[2]

Wanamitindo wa fasheni hutumiwa kwa kuuza mavazi au vipodozi. Watu wanaotengeneza nguo hutumia wanamitindo wa mavazi kuvaa nguo zao na kuoneshea kwenye maonyesho ya mavazi. Wanamitindo hao watatembea juu na chini wakionesha mavazi yao sakafuni panapoitwa en:catwalk au runway kuonyesha nguo hizo kwa watu wengine.[3]

Wanamitindo wa sanaa hukodishwa na wapiga picha, wachoraji na wasanii wengine kwa ajili ya mkao ili kutengeneza sanaa zao.

  1. "history from modelworker". web.archive.org. 2007-10-17. Ilihifadhiwa kwenye nyaraka kutoka chanzo mnamo 2008-02-25. Iliwekwa mnamo 2023-02-26.
  2. "Part(s) Work". 2022.
  3. Walker, Harriet (4 Mei 2009). "Fabulous faces of fashion: A century of modelling". The Independent. Ilihifadhiwa kwenye nyaraka kutoka chanzo mnamo 2011-05-28. Iliwekwa mnamo 2017-09-05.{{cite journal}}: CS1 maint: date auto-translated (link)
Makala hii kuhusu mambo ya utamaduni bado ni mbegu.
Je, unajua kitu kuhusu Mwanamitindo kama historia yake au mahusiano yake na mada nyingine?
Labda unaona habari katika Wikipedia ya Kiingereza au lugha nyingine zinazofaa kutafsiriwa?
Basi unaweza kuisaidia Wikipedia kwa kuihariri na kuongeza habari.