Dini ya Musambwa

Kutoka Wikipedia, kamusi elezo huru
Jump to navigation Jump to search

Dini ya Musambwa ni jumuiya ya kidini iliyoanzishwa na Elijah Masinde kati ya Wabukusu wa Kenya ya magharibi mnamo mwaka 1943. "Musambwa" ni neno la Kibukusu chenye maana ya "roho, pepo".

Elijah Masinde[hariri | hariri chanzo]

Chanzo chake kilikuwa ufunuo ambamo Masinde alisikia sauti ya roho au mungu aliyejitambulisha kwa jina "Wele wa Musambwa". Wito la Musini ilikuwa kuwarudisha Wabukusu kwa dini na utamaduni asilia na kutangaza mwisho wa ukoloni kuwa karibu.

Ibada[hariri | hariri chanzo]

Wafuasi wa Dini ya Musambwa hutazama mlima Elgon kama mlima mtakatifu penye makazi ya roho au mungu huyu. Ibada yao ni kwa mungu Wele na mizimu kwa njia ya sala na sadaka.

Uhusiano na serikali[hariri | hariri chanzo]

Zamani waliambiwa kutolipa kodi na kutosomesha watoto wao kwenye shule za serikali. Kwa sababu kama hizo na upinzani wao dhidi ya serikali ya kikoloni kundi likapgwa marufuku.

Baada ya uhuru likakubaliwa na serikali lakini kwa sababu ya mahubiri ya kisisasa ya Masinde likapigwa marufuku tena.

Baada ya kifo cha Masinde mwaka 1987 idadi ya wafuasi ilipungua lakini kikundi hakikukwisha jinsi walivyotegemea wengine.

Kundi leo[hariri | hariri chanzo]

Katika miaka ya nyuma habari za wafuasi wake walisikika kwenye nafasi mbalimbali.

Mwaka 2001 wafuasi 300 ya 'Dini ya Musambwa' waliripotiwa kuwa walikataa kuchanjwa kwa watoto wao dhidi ya ugonjwa wa polio wakidai ya kwamba chanjo hili lingeudhi amri za imani yao.

Mwaka 2005 wafuasi wa Dini ya Musambwa wakiongozwa na Wamalwa Manai walipinga mipango ya kanisa katoliki la kuhamisha maiti ya marehemu Kardinali Otunga kutoka makaburi yake kwenda bustani ya Resurrection Gardens huko Nairobi wakidai ya kwamba tendo hili lapinga utamaduni wa Kibukusu.

Icon-religion.png Makala hii kuhusu mambo ya dini bado ni mbegu.
Je, unajua kitu kuhusu Dini ya Musambwa kama historia yake au uenezi wake?
Labda unaona habari katika Wikipedia ya Kiingereza au lugha nyingine zinazofaa kutafsiriwa?
Basi unaweza kuisaidia Wikipedia kwa kuihariri na kuongeza habari.