Jimbo Katoliki la Kericho
Mandhari
Jimbo Katoliki la Kericho ni mojawapo kati ya majimbo 28 ya Kanisa Katoliki nchini Kenya. Liko chini ya jimbo kuu la Nairobi.
Makao makuu yako mjini Kericho. Askofu ni Alfred Kipkoech arap Rotich.
Eneo lake ni kilometa mraba 4,800, ambamo mwaka 2023 kati ya wakazi 1,908,510 Wakatoliki walikuwa 294,420 (15.4% ya wakazi wote), wakigawanyika katika parokia 48. Mapadri ni 84, wakiwemo wanajimbo 31 na wanashirika 53. Watawa wa kiume ni 68 na wa kike ni 73.
Tazama pia
[hariri | hariri chanzo]| Makala hii kuhusu Kanisa Katoliki bado ni mbegu. Je, unajua kitu kuhusu Jimbo Katoliki la Kericho kama historia yake au maelezo zaidi? Labda unaona habari katika Wikipedia ya Kiingereza au lugha nyingine zinazofaa kutafsiriwa? Basi unaweza kuisaidia Wikipedia kwa kuihariri na kuongeza habari. |