Jimbo Katoliki la Mtwara
Kutoka Wikipedia, kamusi elezo huru
Jimbo Katoliki la Mtwara (kwa Kilatini Dioecesis Mtuaranus) ni jimbo la Kanisa Katoliki lenye makao makuu mjini Mtwara katika kanda ya Songea upande wa kusini nchi Tanzania.
Kama majimbo yote ya nchi hiyo, linafuata mapokeo ya Roma.
Eneo la jimbo lina kilometa mraba 7,780, ambapo wanaishi wakazi 689,164 (2004), wengi wao wakiwa Waislamu. Kati yao Wakatoliki ni 62,273, sawa na asilimia 9, nao wanaunda parokia 15.
Askofu wa jimbo ni Gabriel Mmole. Mapadri ni 45, ambao kati yao 25 ni wanajimbo na 20 watawa. Kwa wastani kila padri anahudumia waamini 1.383.
Historia[hariri]
- 22 Desemba 1931: Kuundwa kwa Abasia nullius ya Ndanda kutokana na Jimbo Katoliki la Lindi
- 18 Desemba 1972: Kuundwa kama jimbo kamili.
Mlolongo wa Maaskofu[hariri]
- Jimbo la Mtwara
- Askofu Gabriel Mmole (tangu 12 Machi 1988)
- Askofu Maurus Libaba (18 Desemba 1972 – 17 Oktoba 1986)
- Abasia nullius ya Ndanda
- Askofu Anthony Victor Hälg, O.S.B. (15 Desemba 1949 – 1972)
- Askofu Joachim Ammann, O.S.B. (29 Mei 1932 – 15 Desemba 1948)