Yesu Kristo.

Kutoka Wikipedia, kamusi elezo huru
Jump to navigation Jump to search
Yesu Kristo

Yesu Kristo (kutoka Kigiriki Ιησους Χριστός (Iesus Christos) ni jina la kawaida kati ya Wakristo kumuitia Yesu wa Nazareti (Yesu Mnazareti).

Kwa asili ni tamko la imani lenye sehemu mbili: jina "Yesu" na cheo "Kristo".

Kristo ni tafsiri ya Kigiriki ya neno la Kiebrania "mashiah" (Masiya).

Katika lugha ya Kigiriki "Yesu Kristo" mara nyingi ni sentensi kamili, maana yake "Yesu ndiye Masiya wa Mungu", yaani Yesu ndiye Masiya aliyetangazwa na manabii wa Agano la Kale na kutazamiwa na Israeli.

Katika aya nyingine za Agano Jipya "Yesu Kristo" tayari imetumika kama jina. (linganisha: rais Mkapa, au: Mkapa rais - si yule Mkapa mwingine...)

ChristianitySymbol.PNG Makala hii kuhusu dini ya Ukristo bado ni mbegu.
Je, unajua kitu kuhusu Yesu Kristo. kama historia yake, matokeo au athari zake?
Labda unaona habari katika Wikipedia ya Kiingereza au lugha nyingine zinazofaa kutafsiriwa?
Basi unaweza kuisaidia Wikipedia kwa kuihariri na kuongeza habari.