Nenda kwa yaliyomo

Tsavo (mto)

Kutoka Wikipedia, kamusi elezo huru
Muonkeno wa Mto Tsavo kutokea Hifadhi ya Taifa ya Tsavo West .

Tsavo ni jina la mto mmojawapo wa Kenya kusini ambao unatiririka kutoka magharibi hadi mashariki na uko mpakani mwa mbuga ya kitaifa ya milima ya Chyulu, na hifadhi ya Mkomazi nchini Tanzania.

Chanzo chake ni karibu na mpaka wa Tanzania, mguuni pa mlima Kilimanjaro. Unapita Mbuga wa Wanyama wa Tsavo Mashariki na kuishia katika mto Athi karibu na Maporomoko ya maji ya Lugard. Kuanzia hapa mto huitwa Galana.

Mto Tsavo ulijengewa daraja mara ya kwanza wakati wa reli ya Uganda na daraja lile lilikuwa mahali ambako simba waliua wafanyakazi 135.

Hifadhi ya Taifa ya Tsavo Mashariki ni moja ya hifadhi kubwa na kongwe zaidi nchini Kenya iliyotambaa eneo la kilomita za mraba 11,747. Ilifunguliwa mnamo Aprili1948, na iko karibu na kijiji cha Voi katika Wilaya ya Taita-Taveta. Hifadhi hii imetengwa na sehemu ya magharibi na barabara na reli ya A109. Jina lake linatokana na mto Tsavo.

Tazama pia

Tanbihi

Viungo vya nje