Tsavo (mto)

Kutoka Wikipedia, kamusi elezo huru
Jump to navigation Jump to search

Tsavo ni jina la mto mmojawapo wa Kenya. Chanzo chake ni karibu na mpaka wa Tanzania, mguuni pa mlima Kilimanjaro. Unapita Mbuga wa Wanyama wa Tsavo Mashariki na kuishia katika mto Athi karibu na Maporomoko ya maji ya Lugard. Kuanzia hapa mto huitwa Galana.

Mto Tsavo ulijengewa daraja mara ya kwanza wakati wa reli ya Uganda na daraja lile lilikuwa mahali ambako simba waliua wafanyakazi 135.

Viungo vya nje[hariri | hariri chanzo]