Nenda kwa yaliyomo

Aboud Jumbe Mwinyi

Kutoka Wikipedia, kamusi elezo huru
(Elekezwa kutoka Skeikh Mwinyi Aboud Jumbe)

Aboud Jumbe Mwinyi (Unguja, 14 Juni 1920 - Dar es Salaam, 14 Agosti 2016 [1]) alikuwa rais wa pili wa Zanzibar toka tarehe 11 Aprili 1972 hadi 29 Januari 1984 alipojiuzulu[2].

Jumbe alizaliwa kisiwani Unguja mwaka 1920 akasoma shule Zanzibar mjini kuanzia mwaka 1930 hadi 1942. Miaka 1943-1945 alisomea ualimu huko Makerere, Kampala (Uganda) akafundisha shule inayoitwa leo Lumumba College 1946-1960.

Mwaka 1953 alijiunga na chama cha Zanzibar National Union akahamia Chama cha Afro-Shirazi mnamo 1960 akachaguliwa mbunge kwenye mwaka 1961. Akiwa mwakilishi wa upinzani wa ASP, alishiriki kwenye majadiliano kuhusu uhuru wa Zanzibar huko London 1961-1962. [3].

Baada ya mapinduzi ya mwaka 1964 alikuwa waziri katika serikali ya Karume.[4].

Jumbe aliingia madarakani baada ya kuuawa kwa rais wa kwanza Abeid Karume kwenye tarehe 7 Aprili 1972 ambako Jumbe aliteuliwa na Baraza la Mapinduzi kuchukua nafasi yake.

Jumbe aliimarisha uhusiano na Tanzania bara kwa kukubali maungano ya vyama vya TANU na ASP kuwa CCM[5]. Mwaka 1979 Jumbe alitia sahihi katiba ya kwanza ya Zanzibar baada ya mapinduzi iliyomaliza utawala bila kikomo wa Baraza la Mapinduzi; hivyo mwaka 1980 alichaguliwa na raia wa Zanzibar, si wajumbe wa Baraza la Mapinduzi, katika uchaguzi wa kwanza wa Zanzibar tangu mwaka 1963.

Mnamo 1984 Jumbe alidai nafasi kubwa zaidi kwa maazimio ya Zanzibar katika muungano alipaswa kujiuzulu tarehe 29 Januari 1984 wakati wa kikao cha chama cha CCM jijini Dar es Salaam[6].

Jumbe aliaga dunia kwake Kigamboni, Dar es Salaam, tarehe 14 Agosti 2016 akiwa na umri wa miaka 96.[7]

  1. "Nakala iliyohifadhiwa". Ilihifadhiwa kwenye nyaraka kutoka chanzo mnamo 2016-08-15. Iliwekwa mnamo 2016-08-16.
  2. Council on Foreign Relations (1973). The World this Year. Simon and Schuster. ISSN 0364-8575. Iliwekwa mnamo 2015-02-20.
  3. Aboud Jumbe, tovuti ya Munzinger Archiv (Kijerumani), iliangaliwa Julai 2020
  4. M. ABOUD JUMBE DEVIENT VICE-PRÉSIDENT DE LA RÉPUBLIQUE, tovuti ya Le Monde ya tar. 13 Aprili 1972 , iliangaliwa Julai 2020
  5. "CONSTITUTIONALISM AND POLITICAL STABILITY IN ZANZIBAR: THE SEARCH FOR A NEW VISION (PDF)" (PDF). library.fes.de. Iliwekwa mnamo 2015-02-20.
  6. Tanzanian Vice President Aboud Jumbe resigned Sunday from all his posts, tovuti ya UPI Archives Jan. 29, 1984, iliangaliwa Julai 2020
  7. REPORTER, ONLINE. "Former Zanzibar president Mzee Jumbe dies". dailynews.co.tz. Ilihifadhiwa kwenye nyaraka kutoka chanzo mnamo 2016-08-15. Iliwekwa mnamo 2016-08-14.
Alitanguliwa na
Abeid Amani Karume
Makamu wa Rais wa Tanzania
1972-1984
Akafuatiwa na
Ali Hassan Mwinyi
Makala hii kuhusu mwanasiasa fulani bado ni mbegu.
Je, unajua kitu kuhusu Aboud Jumbe Mwinyi kama wasifu wake, habari za maisha au kazi yake?
Labda unaona habari katika Wikipedia ya Kiingereza au lugha nyingine zinazofaa kutafsiriwa?
Basi unaweza kuisaidia Wikipedia kwa kuihariri na kuongeza habari.