Abedi Amani Karume
Mandhari
(Elekezwa kutoka Abeid Amani Karume)
Sheikh Abeid Amani Karume alikuwa Rais wa kwanza wa Zanzibar. Alizaliwa mwaka 1905 na kufariki tarehe 7 Aprili 1972 kwa kupigwa risasi.
Karume aliongoza nchi baada ya mapinduzi yaliyomwangusha Sultani aliyekuwa akitawala Zanzibar hadi mwanzoni mwa mwaka 1964.
Baada ya miezi mitatu Zanzibar iliungana na Tanganyika iliyokuwa ikiongozwa na Mwalimu Nyerere. Baada ya muungano wa nchi hizi mbili uliozaa Tanzania, Karume alikuwa makamu wa rais wa kwanza wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania.
Amani Abeid Karume, ambaye ni mtoto wa Sheikh Karume, alikuwa rais wa Zanzibar tangu mwaka 2000 hadi 2010.
Alitanguliwa na Nafasi ilivyoundwa |
Makamu wa Rais wa Tanzania 1964-1972 |
Akafuatiwa na Mwinyi Aboud Jumbe |