Nenda kwa yaliyomo

Ebola

Kutoka Wikipedia, kamusi elezo huru
(Elekezwa kutoka Mtumiaji:CFCF/sandbox/Ebola)
Ebola virus disease
Mwainisho na taarifa za nje
Kundi MaalumuInfectious diseases Edit this on Wikidata
ICD-10A98.4
ICD-9065.8
DiseasesDB18043
MedlinePlus001339
eMedicinemed/626
MeSHD019142
Picha ya virusi vya Ebola jinsi inayoonekana kwenye hadubini ya elektroni.

Ebola ni ugonjwa unaosababishwa na virusi vya homa ya hemoraji (yaani "kutokwa na damu sana"). Ina kiwango cha juu cha uambukizaji; watu wengi wanaweza kuambukizwa haraka. Huo ugonjwa wa damu kutoganda unaua sana: kati ya watu 10 waliopata virusi vya Ebola, basi wastani kati ya 5 na 9 hufa. Ebola haina chanjo wala tiba lakini kupokea matibabu katika vituo vya Ebola mapema huongeza uwezekano wa kupona.

Namna watu wanavyopata Ebola

[hariri | hariri chanzo]

Wagonjwa wanaweza kuusambaza ugonjwa huu kwa wengine lakini Ebola haiwezi kupatikana kwa njia ya hewa.

Kwa watu, maambukizi hutokea wanapogusa ugiligili wenye virusi hivyo. Wenye Ebola hupata homa ya kumwaga damu sana: wanahara damu na kutapika. Wanatokwa na damu kutoka puani, mdomoni, katika viungo vya uzazi. Uvujaji huo unaweza kuambukiza haraka sana na kusababisha watu wengi wapate virusi.

Watu wanaogusana na wagonjwa wapo katika hatari zaidi: k.mf. jamaa na wahudumu wa afya.

Miili ya wafu pia inaweza kueneza ugonjwa. Hivyo ni lazima kuwa waangalifu: kuzika kwa makini na kukaa mbali. Usioshe, kugusa wala kuibusu maiti. Usinawe mikono kwenye ndoo walionawia watu waliogusa mwili wa mgonjwa.

Kwa kawaida dalili huonekana kati ya siku mbili na ishirini na moja baada ya kuambukizwa. Pale watu wanapopata Ebola, dalili za kwanza ni kuonekana kwa magonjwa mengine: kuwa na homa, uchovu, kichefuchefu, maumivu ya koo, tumbo, musuli, kichwa na viungo vingine. Kwa dalili hizo, watu hufikiria kwamba wana magonjwa mengine kama vile malaria au homa ya matumbo.

Kwa kawaida hali inayofuata ni kichefuchefu, matapishi yanayoweza kuwa na damu, kikohozi pia kinaweza kuwa na damu, harisho (pengine lenye damu) pamoja na figo kutofanya kazi vizuri, huku watu wengine huanza kutokwa na damu.

Baadaye, hali inakuwa mbaya zaidi, hadi kufikia hali ya kumwaga damu kwa kiasi kikubwa sana. Wanapata mshtuko: shinikizo la damu kuwa chini, mapigo ya moyo kwenda kasi, na mzunguko wa damu kuwa hafifu mwilini. Hii inasababisha viungo vya mwili kuuma sana na kuacha kufanya kazi.

Ebola pia husababisha ukakamavu mwilini ambapo inawaacha waathirika kitandani. Hata kama watafanikiwa kufika hospitalini, wengi wao hufa.

Chanzo na utambuaji

[hariri | hariri chanzo]

Chanzo pamoja na utambuaji wa virusi huenda inaambukiza kutokana na kugusa damu au majimaji ya ngedere anayeambukiza. Pia popo wa matunda hubeba maradhi ingawa hawaambukizwi. Wanyama hao wawili huambukiza zaidi kuliko wengine. Kama virusi hiyo hubebwa na upepo haijathibitishwa na wataalamu wakifanya utafiti katika mazingira ya asili.

Binadamu wakishaambukizwa wanaweza kuwaambukiza wengine. Wanaume walioambukizwa wanaweza kuwaambukiza wengine wakifanya ngono nao huku madhii inabeba virusi. Hatari hii huweza kudumu kwa takriban miezi miwili.

Mkakati wa utambuaji kwanza unalenga kuitofautisha ebola na maradhi ya malaria na kipindupindu yakiwa na mengine yenye homa zivujazo damu. Ili kuthibitisha utambuaji, sampuli zinachunguzwa kubainisha zindiko au virusi za RNA ama virusi yenyewe ya ebola.

Ebola huhesabiwa kati ya magonjwa ya mlipuko. Inaweza kuambukiza kutoka kwa mgonjwa au maiti.

Hivyo wagonjwa wa Ebola hutenganishwa na wagonjwa wengine wasije wakawaambukiza. Hii ina maana kwamba watu wengine wasije wakagusa ugiligili na damu yao. Basi watu wengine hawawezi kupata virusi hii kwa sababu tayari hatua ya kuwatenganisha imeshapita.

Ili kuzuia usambazaji wa ebola vitendo vifuatavyo vitendeke: 1. Ebola huwaambukiza wanyama na popo pia. Usiguse wala kula "nyama ya msituni" au popo. Ngedere walioambukizwa watafutwe wakauawe na mizoga yao ichomwe moto. 2. Kuipika vizuri nyama huku mpishi awe katika hali ya usafi kabisa akivaa sare ifaavyo kumkinga kabisa. Ni lazima mpishi anawe mikono kabla ya kugusa nyama ama vifaa vya upishi, pia ni muhimu kujihadhari kwa kunawa ukiwa karibu na mtu anayeambukizwa. 3. Sampuli ya majimaji ya kimwili pamoja na tishu kutoka kwa walioambukizwa lazima ziguswe taratibu sana.

Usimguse mgonjwa au mtu aliyekufa wala viowevu vya mwili wake: damu, matapishi, mkojo, kinyesi au kuhara. Nawa mikono mara kwa mara kwa kutumia sabuni; iwapo huwezi kunawa, pangusa na jeli ya alkoholi. Safisha nyumba yako kwa sehemu 1 ya dawa ya kung’arisha na sehemu 9 ya maji.

Mtu akifariki kutokana na Ebola akiwa nyumbani mwako, usiguse mwili, malazi au viowevu vya mwili wake. Kaa mita 1 mbali na maiti. Umpigie simu mhudumu wa afya. Uwaruhusu wahudumu wa afya kufika nyumbani mwako washughulikie mwili huo na wasafishe nyumba kwa kuinyunyizia klorini.

Waliofariki kwa Ebola lazima wazikwe haraka. Uende na wahudumu wa afya kwenye eneo la kaburi. Epuka kushiriki chakula, kinywaji na kunawa mikono kwa pamoja wakati wa mazishi. Kawisha sherehe za baada ya mazishi hadi baadaye katika mwaka. Nyumba ikiwa safi ni salama kwako kurudi.

Hatua za kuchukua ukiambukizwa

[hariri | hariri chanzo]
  • Piga simu kwenye kituo chako cha matibabu uwaeleze kuhusu ugonjwa wako.
  • Sikiliza maoni yao. Huenda ukatumwa hadi hospitali maalum.
  • Kaa mbali na watu wengine ili nao wasiambukizwe.
  • Hasa kuwa mwangalifu na matapishi na kinyesi chako.

Habari hii haikusudiwi kutumika badala ya ushauri wa kimatibabu. Iwapo una maswali yoyote kuhusu mada yoyote iliyozungumziwa humu, tafadhali pata ushauri wa mtalaamu wa afya.

Tiba na chanjo

[hariri | hariri chanzo]

Pale mlipuko unapotokea, watu wengi huja na kujaribu kusaidia kuzuia. Shirika la Afya Duniani ni moja kati ya makundi muhimu sana kwa jitihada zake za kujaribu kuzuia mlipuko wa ugonjwa wa Ebola.

Mpaka leo hii hakuna tiba maalumu ya homa ya Ebola. Lakini ikiwa watu wanapata huduma bora kutoka kwa madaktari na wauguzi, wengi wao huishi.

Jitihada za kuwasaidia walioambukizwa ni pamoja na kuwapa tiba yenye uunganaji kikemikali na maji mdomoni (wanywe maji matamu kidogo pamoja na maji yenye chumvi) au kupata kwa njia ya sindano ya vena. Huduma bora kwao inaweza kuwa kwa ugiligili au damu zinazotolewa kwa vena za watu. Inaweza kuwa dawa za kufanya shinikizo la damu na mzunguko wa damu vifanye kazi vizuri.

Bidii zinafanyika katika utafutaji wa dawa ya chanjo, lakini hadi leo hii hakuna.

Matarajio

[hariri | hariri chanzo]

Kiwango cha vifo ni cha juu sana: idadi ya waambukizwa wanaokufa ni kati ya 50% na 90%.

Milipuko

[hariri | hariri chanzo]

ETB ilitokea kwa mara ya kwanza nchini Sudan pamoja na Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo. Kwa kawaida ugonjwa huu huibuka katika sehemu za joto jingi za Afrika zilizoko kusini kwa Jangwa la Sahara.

Kuanzia mwaka 1976 (ilipotambulika kwa mara ya kwanza) hadi 2013 idadi ya watu walioambukizwa ilikuwa chini ya elfu moja kwa mwaka.

Mlipuko mkubwa hadi leo hii ni ile inayoendelea hasa katika nchi za Liberia, Sierra Leone na Guinea (Mlipuko wa 2014 wa Ebola Afrika).

Hadi mwezi Novemba 2014 wagonjwa wapatao 15,000 walitambuliwa kuambukizwa, na kati yao 5,000 walikwishakufa.

Hatimaye mlipuko huo ulimalizika mnamo Januari 2016 baada ya kuua watu 11,000.

  • Klenk, Hans-Dieter (1999). Marburg and Ebola Viruses (Current Topics in Microbiology and Immunology). Berlin, Germany: Springer-Verlag Telos. ISBN 978-3540647294. {{cite book}}: Unknown parameter |month= ignored (help)CS1 maint: ref duplicates default (link)
  • Klenk, Hans-Dieter; Feldmann, Heinz (2004). Ebola and Marburg viruses: molecular and cellular biology (Limited preview). Wymondham, Norfolk, UK: Horizon Bioscience. ISBN 978-0954523237.{{cite book}}: CS1 maint: ref duplicates default (link)
  • Kuhn, Jens H. (2008). Filoviruses – A Compendium of 40 Years of Epidemiological, Clinical, and Laboratory Studies. Archives of Virology Supplement, vol. 20 (Limited preview). Vienna, Austria: SpringerWienNewYork. ISBN 978-3211206706.{{cite book}}: CS1 maint: ref duplicates default (link)
  • McCormick, Joseph; Fisher-Hoch, Susan (1999) [1996]. Level 4: Virus Hunters of the CDC (Limited preview). Horvitz, Leslie Alan (tol. la "Updated edition" 3rd). Barnes & Noble. ISBN 9780760712085. {{cite book}}: Unknown parameter |month= ignored (help)CS1 maint: ref duplicates default (link)
  • Pattyn, S. R. (1978). Ebola Virus Haemorrhagic Fever (tol. la 1st). Amsterdam, Netherlands: Elsevier/North-Holland Biomedical Press. ISBN 0-444-80060-3. Ilihifadhiwa kwenye nyaraka kutoka chanzo (Full free text) mnamo 2010-12-11. Iliwekwa mnamo 2010-11-13. {{cite book}}: Unknown parameter |= ignored (help)CS1 maint: ref duplicates default (link)
  • Ryabchikova, Elena I.; Price, Barbara B. (2004). Ebola and Marburg Viruses – A View of Infection Using Electron Microscopy. Columbus, Ohio, USA: Battelle Press. ISBN 978-1574771312.{{cite book}}: CS1 maint: ref duplicates default (link)

Viungo vya nje

[hariri | hariri chanzo]