Majadiliano:Ebola
Mandhari
Naona tunatofautiana kuhusu virusi: ni wingi wa kirusi au ni umoja pia? Kidahizo chake virusi kinafikia kusema "virusi cha"... --Riccardo Riccioni (majadiliano) 11:40, 15 Agosti 2014 (UTC)
- Kwangu haina maana kubuni neno kama "kirusi" (maana yake ni "Russian" si ndiyo?). "Virusi" inatoka Kiingereza na ninaichukulia kama nomino ya 9/10. Lakini niliona kwamba watu wengine hutumia kirusi/virusi. Mantiki yao ni nini? ChriKo (majadiliano) 22:28, 17 Agosti 2014 (UTC)
- Kamusi ya TUKI imeandika "virusi, ngeli 9/10". Hata hivyo, mantiki ya wasemaji wasemao "kirusi" kwa umoja ni analojia, na ndiyo sababu inawezekana kusikia kideo/video, kirusi/virusi na kipilefti/vipilefti. Haya, mambo ya "prescriptive" na "descriptive" :) --Baba Tabita (majadiliano) 18:21, 18 Agosti 2014 (UTC)