Ebola

Kutoka Wikipedia, kamusi elezo huru
Rukia: urambazaji, tafuta
Picha ya virusi ya Ebola jinsi inayoonekana kwenye hadubini ya elektroni.

Ebola ni ugonjwa unaosabibishwa na virusi fulani ya homa ya hemoraji (yaani "kumwaga damu sana"). Huo ugonjwa wa damu kutoganda unaua sana. Kati ya watu 10 waliopata virusi ya Ebola, basi wastani kati ya watano na tisa hufa.

Namna watu wanavyopata Ebola[hariri | hariri chanzo]

Katika watu, maambukizi hutokea mtu anapogusa ugiligili wenye virusi. Ebola haiwezi kupatikana kwa njia ya hewa. Watu wenye Ebola hupata homa ya kumwaga damu sana: wanahara damu na kutapika. Wanamwaga damu kutoka puani, mdomoni, katika viungo vya uzazi. Uvujaji huo unaweza kuambukiza haraka sana na kusababisha watu wengi wapate virusi.

Dalili za Ebola[hariri | hariri chanzo]

Pale watu wanapopata Ebola, dalili zake za kwanza ni kuonekana kwa magonjwa mengine. Watu wanapata homa, kujisikia kuchoka, maumivu ya kichwa, maumivu ya tumbo, maumivu katika viungo vyao, na maumivu kooni. Kwa dalili hizo, watu hufikiria kwamba wana magonjwa mengine kama vile malaria au homa ya matumbo.

Baadaye, hali inakuwa mbaya zaidi, hadi kufikia hali ya kumwaga damu kwa kiasi kikubwa sana. Wanapata mshtuko: shinikizo la damu kuwa chini, mapigo ya moyo kwenda kasi, na mzunguko wa damu kuwa hafifu mwilini. Hii inasababisha viungo vya mwili kuuma sana. Viungo vya mwili vinaacha kufanya kazi.

Ebola pia husababisha ukakamavu mwilini ambapo inawaacha waathirika kitandani. Hata kama watafanikiwa kufika hospitalini, wengi wao hufa.

Tiba ya Ebola[hariri | hariri chanzo]

Hakuna tiba maalumu ya homa ya Ebola. Lakini ikiwa watu wanapata huduma bora kutoka kwa madaktari na wauguzi, wengi wao huishi. Huduma bora kwao inaweza kuwa kwa ugiligili au damu zinazotolewa kwa vena za watu. Inaweza kuwa dawa za kufanya shinikizo la damu na mzunguko wa damu vifanye kazi vizuri.

Ebola huhesabiwa kati ya magonjwa ya mlipuko.

Wagonjwa wa Ebola hutenganishwa na wagonjwa wengine ili wasipate kuwaambukiza. Hii ina maana kwamba watu wengine wasije wakagusa ugiligili na damu yao. Basi watu wengine hawawezi kupata virusi hii kwa sababu tayari hatua ya kuwatenganisha imeshapita.

Pale mlipuko unapotokea, watu wengi huja na kujaribu kusaidia kuzuia. Shirika la Afya Duniani ni moja kati ya makundi muhimu sana kwa jitihada zake za kujaribu kuzuia mlipuko wa ugonjwa wa Ebola.

Tanbihi[hariri | hariri chanzo]

Marejeo[hariri | hariri chanzo]

Viungo vya Nje[hariri | hariri chanzo]