Nenda kwa yaliyomo

Mkoa wa Tabora

Kutoka Wikipedia, kamusi elezo huru


Mkoa wa Tabora
Mahali paMkoa wa Tabora
Mahali paMkoa wa Tabora
Mahali pa Mkoa wa Tabora katika Tanzania
Majiranukta: 5°30′S 32°50′E / 5.500°S 32.833°E / -5.500; 32.833
Nchi Tanzania
Wilaya 6
Mji mkuu Tabora
Serikali
 - Mkuu wa Mkoa Abeid Mwinyimsa
Eneo
 - Jumla 75,264 km²
Idadi ya wakazi (2002)
 - Wakazi kwa ujumla 1,717,908
Tovuti:  http://www.tabora.go.tz/

Tabora ni jina la mji, wilaya na mkoa wa Tanzania ya kati.

Mkoa wa Tabora iko kati ya mikoa 26 ya Tanzania. Makao makuu yako Tabora Mjini.

Eneo la mkoa ni 76,151 km² mnamo 34,698 km² (46%) ni hifadhi ya misitu, 17,122 km² (22%) ni hifadhi ya wanyama. Wakazi walio wengi ni wakulima na wafugaji. Jumla ya wakazi ilikuwa watu 1,717,908 (mw. 2002).

Ramani ya Mkoa wa Tabora

Kuna wilaya 6 (idadi ya wakazi kwa mabano): Tabora Mjini (188,808), Nzega (417,097), Igunga (325,547), Uyui (282,272), Urambo (370,796), Sikonge (133,388).

Tabora haina barabara za lami. Kuna njia ya reli ya kati kutoka Daressalaam kwenda Kigoma kwa upande moja na kwenda Mwanza kwa upande mwingine.

Jina la Urambo humkumbuka Mtemi Mirambo aliyekuwa mtwala muhimu wa Wanyamwezi kabla ya kuingia kwa ukoloni.

Wenyeji wa Tabora ni hasa Wanyamwezi.