Nenda kwa yaliyomo

Mikoa ya Senegal

Kutoka Wikipedia, kamusi elezo huru
Mikoa ya Senegal

Mikoa ya Senegal ni ngazi ya kwanza ya ugatuzi nchini Senegal katika Afrika ya Magharibi. Senegal imegawanywa katika mikoa 14 (kwa Kifaransa: régions). Kila mkoa unasimamiwa na halmashauri yake (Conseil Régional) ambayo wajumbe wake wanachaguliwa na wananchi kwenye ngazi ya tarafa.

Ngazi ya pili ya ugatuzi ni wilaya (departements) 45, tarafa (arrondissements) 103 (ambazo hazina kazi ya kiutawala) na maeneo ya jumuiya za kieneo (collectivités locales) ambazo huchagua maafisa wa utawala.

Orodha ifuatayo inaonyesha mikoa ya Senegal pamoja na idadi ya wakazi kufuatana na sensa ya mwaka 2013.[1]

Mkoa Makao makuu Eneo
(km²)
Wakazi
(sensa 2013)
DakarDakar5473,137,196
ZiguinchorZiguinchor7,352549,151
DiourbelDiourbel4,8241,497,455
Saint-LouisSaint-Louis19,241908,942
TambacoundaTambacounda42,364681,310
KaolackKaolack  5,357960,875
ThièsThiès6,6701,788,864
LougaLouga24,889874,193
FatickFatick6,849835,352
KoldaKolda13,771714,392
MatamMatam29,445562,539
KaffrineKaffrine11,262566,992
KédougouKédougou16,800152,357
SédhiouSédhiou7,341452,944
Jengo la Halmashauri ya Mkoa huko Ziguinchor. Mikoa huwa na madaraka ya kikatiba nchini Senegal, tofauti na wilaya na tarafa.
  1. Senegal: Administrative Division, tovuti ya Citypopulation.de, iliangaliwa Januari 2022