Mkoa wa Diourbel

Kutoka Wikipedia, kamusi elezo huru
Mahali pa Mkoa wa Diourbel nchini Senegal
Wilaya za Diourbel

Mkoa wa Diourbel (kwa Kiserer: Jurbel) ni mkoa wa Senegal. Makao makuu ya mkoa yako mjini Diourbel.

Mkoa una eneo la kilomita za mraba 4,824 lililokaliwa na wakazi 1,497,455 wakati wa sensa ya mwaka 2013.[1]

Eneo hilo linalingana takriban na ufalme wa Bawol uliotawala hapa kabla ya ukoloni na bado linaitwa jina hilo. [2] Wakazi wa eneo hilo wanaitwa Bawol-Bawol.

Wakazi walio wengi ni Waserer [3] ambao wanatazamwa kuwa wenyeji wa eneo hili. [4] Wawolof na makabila mengine wapo pia.

Mkoa wa Diourbel una historia tajiri na ndipo mahali ambapo vinapatikana vichuguu vya Cekeen ambavyo ni makaburi ya wafalme wa kale na kuheshimiwa kama mahali patakatifu katika dini asilia ya Waserer.

Mji mtakatifu wa Touba wenye kaburi la shehe Ahmadou Bàmba Mbàcke umo mkoani na wafuasi wengi wa jumuiya ya Wamuridi wanakuja kusali kwenye kaburi la shehe.[5]

Wilaya[hariri | hariri chanzo]

Mkoa wa Diourbel unajumuisha wilaya (departements) tatu:

Marejeo[hariri | hariri chanzo]

  1. Senegal: Administrative division, tovuti ya citypopulation.de
  2. Institut fondamental d'Afrique noire, Bulletin de l'Institut fondamental d'Afrique noire, Volume 38.
  3. Klein, Martin A, "Islam and Imperialism in Senegal Sine-Saloum, 1847-1914", Edinburgh University Press (1968), p 5
  4. Gastellu, Jean-Marc, "L'Egalitarisme économique des Serer du Sénégal", IRD Editions (1981), p 446, ISBN 2709905914 [1] (Retrieved : 10 July 2012)
  5. taz. Gastellu

Viungo vya nje[hariri | hariri chanzo]