Mkoa wa Tambacounda

Kutoka Wikipedia, kamusi elezo huru
Mahali pa Tambacounda nchini Senegal
Wilaya za Tambacounda

Mkoa wa Tambacounda ni mkoa mmojawapo wa Senegal. Zamani ikijulikana kama Sénégal Oriental (Senegal ya Mashariki).

Mkoa una eneo la kilomita za mraba 42,364 lililokaliwa na wakazi 681,310 wakati wa sensa ya mwaka 2013.[1] Mkoa una mipaka ya kimataifa na Mali, Guinea na Gambia.

Eneo lake lilikuwa sehemu ya Milki ya Mali kabla ya kuchorwa kwa mipaka ya kikoloni iliyotenganisha Mali na Senegal.

Tambacounda ni mkoa mkubwa zaidi nchini Senegal, lakini ina wakazi wachache na uchumi wake uko nyuma ya mikoa mingine. Wilaya ya Kédougou ilitenganishwa na Tambacounda mwaka 2008 na kuwa mkoa wa pekee.

Wilaya[hariri | hariri chanzo]

Mkoa wa Tambacounda umegawanywa katika wilaya 4:

  • Wilaya ya Bakel
  • Wilaya ya Goudiry
  • Wilaya ya Koumpentoum
  • Wilaya ya Tambacounda

Uchumi[hariri | hariri chanzo]

Uchumi wa Tambacounda unategemea zaidi kilimo. Mazao ya biashara ni pamoja na pamba na karanga. Uchimbaji madini una jukumu katika sehemu ya kusini ya eneo karibu na mji la Kedougou. Kanda hiyo pia ni nyumbani kwa Mbuga wa Kitaifa wa Niokolo-Koba ambao ni hifadhi kubwa zaidi katika Afrika ya Magharibi. Hivyo utalii una umuhimu pia katika uchumi wa mkoa. [2]

Marejeo[hariri | hariri chanzo]

  1. Senegal: Administrative division, tovuti ya citypopulation.de
  2. Anthony Ham (2010). Lonely Planet Africa. Lonely Planet. pp. 496–497. ISBN 978-1-74104-988-6.  Unknown parameter |url-access= ignored (help)