Mikoa ya Mali
Mikoa ya Mali ni magatuzi ya nchi ya Mali kwenye ngazi ya juu. Tangu mwaka 2016 Mali imegawanywa katika mikoa kumi na eneo la pekee la mji mkuu.
Mnamo mwaka 2012 sheria ilitangaza kugawiwa upya kwa nchi katika mikoa 19 kutoka ile 8 ya awali[1]. Hadi mwaka 2021 kuna mikoa miwili mipya pekee iliyoanzishwa, ambayo ni Taoudenit (iliyomegwa kutoka Mkoa wa Timbuktu) na Menaka (zamani kwenye Mkoa wa Gao).[2] [3]
Kila mkoa unaitwa jina la mji mkuu wake. Mikoa imegawanywa katika wilaya (cercles) 56. Wilaya zote zimegawanywa katika manispaa (communes) 703. [4]
Jiografia
Mikoa 5 ni hasa jangwa, na mikoa hiyo ina nusu ya eneo lote la nchi.
Mkoa mkubwa zaidi ni Taoudenit, mdogo zaidi ni Segou.
Demografia
Mkoa wenye watu wengi zaidi ni Sikasso wenye watu milioni 2.6, na ule wenye watu wachache zaidi una watu 68,000 pekee.
Mikoa
Mikoa imepewa namba kwa kutumia namba za Kiroma.[5] Mji mkuu wa Bamako unasimamiwa kama eneo la pekee.
Mikoa kumi na eneo la Bamako vimeorodheshwa hapa chini. Idadi ya wakazi ni kutokana na sensa za 1998 na 2009. [6]
Jina la mkoa | Nambari ya mkoa | Eneo (km2) | Idadi ya watu Sensa ya 1998 |
Idadi ya watu Sensa ya 2009 |
---|---|---|---|---|
Kayes | I | 119,743 | 1,374,316 | 1,993,615 |
Koulikoro | II | 95,848 | 1,570,507 | 2,422,108 |
Bamako | (bila namba) | 252 | 1,016,296 | 1,810,366 |
Sikasso | III | 70,280 | 1,782,157 | 2,643,179 |
Segou | IV | 64,821 | 1,675,357 | 2,338,349 |
Mopti | V | 79,017 | 1,484,601 | 2,036,209 |
Timbuktu[7] | VI | 496,611 | 442,619 | 674,793 |
Gao | VII | 89,532 | 341,542 | 542,304 |
Kidal | VIII | 151,430 | 38,774 | 67,739 |
Taoudénit | IX | - | - | - |
Ménaka | X | 81,040 | - | - |
Marejeo
- ↑ "LOI No 2012-017 DU 02 MARS 2012 PORTANT CREATION DE CIRCONSCRIPTIONS ADMINISTRATIVES EN REPUBLIQUE DU MALI" (PDF). Journal officiel de la République du Mali. 2 Machi 2012. Ilihifadhiwa kwenye nyaraka kutoka chanzo (PDF) mnamo 2018-11-23. Iliwekwa mnamo 21 Februari 2017.
{{cite web}}
: CS1 maint: date auto-translated (link) - ↑ "Régionalisation: Deux Nouvelles régions créées au Mali". Malijet. 21 Januari 2016. Ilihifadhiwa kwenye nyaraka kutoka chanzo mnamo 2017-02-22. Iliwekwa mnamo 21 Februari 2017.
{{cite web}}
: CS1 maint: date auto-translated (link) - ↑ "Report of the Secretary-General on the situation in Mali" (PDF). MINUSMA. 28 Machi 2016. Iliwekwa mnamo 21 Februari 2017.
{{cite web}}
: CS1 maint: date auto-translated (link) - ↑ Loi N°99-035/ Du 10 Aout 1999 Portant Creation des Collectivites Territoriales de Cercles et de Regions (PDF) (kwa Kifaransa), Ministère de l'Administration Territoriales et des Collectivités Locales, République du Mali, 1999, ilihifadhiwa kwenye nyaraka kutoka chanzo (PDF) mnamo 2012-03-09.
- ↑ Évaluation de la coopération décentralisée franco-malienne La coopération décentralisée franco-malienne, état des lieux Ilihifadhiwa 14 Februari 2012 kwenye Wayback Machine., Ministère des Affaires étrangères et européennes (French Ministry of Foreign Affairs).
- ↑ Resultats Provisoires RGPH 2009 (PDF) (kwa Kifaransa), République de Mali: Institut National de la Statistique, ilihifadhiwa kwenye nyaraka kutoka chanzo (PDF) mnamo 2020-01-11, iliwekwa mnamo 2022-01-09
{{citation}}
: Unknown parameter|dead-url=
ignored (|url-status=
suggested) (help). - ↑ Namba za Timbuktu bado pamoja na eneo na wakazi wa mkoa mpya wa Taoudenit uliotengwa hapa mwaka 2016