Nenda kwa yaliyomo

Mkoa wa Segou

Kutoka Wikipedia, kamusi elezo huru
Mashamba, sahel, na mabwawa ya mito karibu na Macina, Mkoa wa Ségou

Mkoa wa Segou (kwa Kibambara: Segu Dineja) ni mkoa wa kiutawala nchini Mali, uliopo katikati mwa nchi hiyo. Eneo lake ni km2 64,821. Mkoa huu umepakana na mikoa ya Sikasso upande wa kusini, Timbuktu na Mopti upande wa mashariki, Burkina Faso kwa upande wa kusini mashariki na Mkoa wa Koulikoro upande wa magharibi. Mwaka 2009 iddai ya wakazi ilikuwa 2,336,255. Makao makuu ya kiutawala yapo mjini Segou .

Tabianchi[hariri | hariri chanzo]

Mkoa wa Segou una tabianchi ya nusu yabisi. Wastani wa mvua kwa mwaka ni milimita 513. Mito ya Niger na Bani inapita mkoa huo na kuruhusu umwagiliaji kwa kilimo . Segou ina misimu miwili: msimu wa mvua na kiangazi. Msimu wa mvua huanza Juni na hudumu takriban miezi minne hadi Septemba. Kwa upande mwingine, msimu wa kiangazi hujumuisha kipindi cha baridi na kipindi cha joto. Upepo wa Harmattan ni upepo unaotawala kipindi cha kiangazi na huvuma kutoka kaskazini hadi kusini. Monsuni inayovuma kutoka kusini hadi kaskazini-magharibi inapatikana zaidi wakati wa msimu wa mvua. [1]

Demografia[hariri | hariri chanzo]

Wakazi wa mkoa ni ama wakulima au wafugaji wa kuhamahama. Makabila ni mengi, pamoja na Wabambara, Wabozo, Wasoninke, Wamalinke na Watoucouleur. Wabambara wengi wao ni wakulima na ndio kabila lililo na watu wengi zaidi.

Wabozo ni kabila la pili kwa idadi ya watu. Wanaishi kando la mto Niger ambao ni wavuvi. Wanaendesha pia usafirishaji kwenye maji.

Wasomono si kabila tofauti bali ni mchanganyiko wa Wabambara, Wabozo na Wasoninke wanaokaa pamoja karibu na mto na kufanya uvuvi. Wamalinke, Maninka, na Wamandinka wana uhusiano wa karibu na Wabambara. Mavazi, imani na desturi za kidini ni sawa na Wabambara.

Uchumi[hariri | hariri chanzo]

Segou inajulikana kwa ufinyanzi wake na tasnia ya uvuvi.

Kilomita 10 kutoka makuu uko mji wa kihistoria wa Segou-Koro uliokuwa mji mkuu wa Milki ya Bambara penye majengo ya kale.

Shughuli kuu za kiuchumi za eneo la Segou ni biashara ya kilimo, ufugaji wa ng'ombe na uvuvi. Watu wa Ségou hutumia mbinu za kilimo cha kitamaduni. Srgou inazalisha sehemu kubwa ya chakula cha kitaifa cha Mali.

Wakazi wengi wanalima ili kujikimu. Kuna viwanda vitatu vya vyakula ambavyo ni COMATEX, CMDT na SUKALA. Wakulima wadogo huuza mazao kila wiki kwenye soko kubwa la Segou linalovuta wateja kutoka mbali. Bidhaa kuu zinazouzwa ni mboga, vyombo vya ufinyanzi, pamba, dhahabu, ngozi, matunda, ng'ombe na nafaka. [2]

Wilaya[hariri | hariri chanzo]

Wilaya za Mkoa wa Ségou

Mkoa wa Ségou umegawanywa katika wilaya (cercles) 7 zinazojumuisha halmashauri 118 na vijiji 2,166: [3]

Jina la Cercle Eneo (km2) Idadi ya watu
Sensa ya 1998
Idadi ya watu
Sensa ya 2009
Bla 6,200 202,295 283,663
Baroueli 4,170 157,145 203,550
Macina 11,750 168,853 237,477
Niono 23,063 228,264 365,443
San 7,262 250,597 334,911
Segou 10,844 501,447 691,358
Tominian 6,573 166,756 219,853

Miji[hariri | hariri chanzo]

Miji mikubwa ni Segou, San, Niono, Dioro, na Markala, ambako kuna bwawa la kuzalisha umememaji .

Historia[hariri | hariri chanzo]

Eneo hilo lilikuwa kitovu cha Milki ya Bambara mwanzoni mwa karne ya 18. Ilitekwa na Dola ya Toucouleur katika miaka ya 1860 na Ufaransa katika miaka ya 1890.

Marejeo[hariri | hariri chanzo]

  1. Caractéristiques physiques Retrieved May 29, 2007 from http://region.segou.net/caracteristique.htm
  2. Activités économiques.
  3. Communes de la Région de Ségou (PDF), Ministère de l’administration territoriale et des collectivités locales, République du Mali, ilihifadhiwa kwenye nyaraka kutoka chanzo (PDF) mnamo 2012-03-09.

Viungo vya nje[hariri | hariri chanzo]