Nenda kwa yaliyomo

Mkoa wa Koulikoro

Kutoka Wikipedia, kamusi elezo huru
Ramani ya Mkoa wa Koulikoro.

Mkoa wa Koulikoro (Kibambara : Kulikoro Dineja) ni mkoa ulioko magharibi mwa Mali . Ni eneo la kilomita za mraba 90,120. Makao makuu yake ni mji wa Koulikoro. Eneo la mji mkuu wa kitaifa Bamako liko ndani ya eneo la mkoa huo lakini linautawala wa pekee si sehemu ya mkoa.

Jiografia

[hariri | hariri chanzo]

Mkoa wa Koulikoro limepakana na Mauritania upande wa kaskazini, Mkoa wa Kayes upande wa magharibi, Guinea na Mkoa wa Sikasso upande wa kusini na Mkoa wa Segou upande wa mashariki. Mwaka 2009 Mkoa wa Koulikoro ulikuwa na wakazi 2,418,305. Hawa walikuwa hasa Wabambara, Wamalinke, Wasonike na Wasomono wanaokaa kando la Mto Niger .

Mito ni pamoja na Niger, Baoule, Sankarani, Baoge, Bani na Bafing. Tabianchi ya eneo ya kusini ya mkoa ina mvua nyingi lakini kaskazini mwa kuna ukame.

Miji mikubwa zaidini Kati, Koulikoro, Kolokani, Nara, Banamba na Dioïla. Halmashauri yenye wakazi wengi ni Kalabancoro.

Historia

[hariri | hariri chanzo]

Mkoa wa Koulikoro ulikuwa eneo ambako milki kubwa kadhaa katika historia ya Mali zilianza: Dola la Ghana, Milki ya Sosso na Milki ya Mali .

Usafiri na uchumi

[hariri | hariri chanzo]

Koulikoro ni mwisho wa njia ya reli kutoka Dakar hadi mto Niger. Ni pia bandari muhimu kwenye mto Niger inayohudumia pia miji ya Segou, Mopti, Timbuktu na Gao.

Kilimo ni shughuli kuu ya kiuchumi, lakini kuna pia viwanda kadhaa vipo katika mkoa huo, kama vile lamba la umememaji la Selingue, uzalishaji wa dhahabu karibu na Kangaba, na eneo la uzalishaji wa pamba huko Fana, ambalo ni la pili kwa ukubwa nchini Mali.

<i id="mwVg">Cercles</i> katika Mkoa wa Koulikoro

Mkoa wa Koulikoro umegawiwa kwa wilaya 7 zinazoitwa cercles zinazojumuisha halmashauri (communes) 106 : [1]

Jina la Cercle Eneo (km2) Idadi ya watu 1998 Idadi ya watu</br> Sensa ya 2009
Nara 30,000 166,783 242,990
Banamba 7,500 142,160 190,235
Kolokani 12,000 184,905 233,919
Koulikoro 7,260 153,485 211,103
Dioila 12,794 332,972 491,210
Kati 16,897 513,798 948,128
Kangaba 5,500 76,404 100,720

Bamako ambayo ni mji mkuu wa Mali iko katikati ya mkoa huo, lakini ni eneo la pekee la kiutawala. Linazungukwa na Cercle ya Kati.

  1. Communes de la Région de Koulokoro (PDF) (kwa Kifaransa), Ministère de l’administration territoriale et des collectivités locales, République du Mali, ilihifadhiwa kwenye nyaraka kutoka chanzo (PDF) mnamo 2012-03-09.

Viungo vya nje

[hariri | hariri chanzo]