Nenda kwa yaliyomo

Mkoa wa Kayes

Kutoka Wikipedia, kamusi elezo huru
Mkoa wa Kayes. Barabara zisizo na lami zinaonyeshwa kwa njia zenye mistari. Mipaka ya Hifadhi ya Kitaifa ya Boucle du Baoulé ni takriban.
Cercles za Mkoa wa Kayes

Mkoa wa Kayes (kwa Kibambara: Kayi Dineja) ni mojawapo ya mikoa nane nchini Mali inayoitwa regions. Eneo lake ni kilomita za mraba 120,760. Idadi ya wakazi ilikuwa takriban milioni 2 kwenye mwaka 2009. Makao makuu yako mjini Kayes . Mkoa huo kihistoria ulikuwa sehemu ya Dola la Ghana na Milki ya Mali.

Jiografia[hariri | hariri chanzo]

Mkoa wa Kayes umepakana na Mauritania upande wa kaskazini, Senegal upande wa magharibi, Guinea upande wa kusini na upande wa mashariki uko Mkoa wa Koulikoro .

Makabila ya eneo hilo ni pamoja na Wasoninke, Wakhassonke, Wamalinke, Wadialonke na Wafulani.

Mito ya mkoa ni pamoja na Baoule, Bafing na Bakoy ambayo inaungana katika mji wa Bafoulabe kuunda Mto Senegal.

Miji mikubwa katika eneo ni Kayes, Kita, Bafoulabé, Nioro du Sahel, Diéma, Yélimané, Sadiola na Kéniéba.

Wilaya[hariri | hariri chanzo]

Mkoa wa Kayes umegawiwa katika wilaya 7 zinazoitwa cercles: [1]

Jina la Cercle Eneo (km2) Idadi ya watu 1998 Idadi ya watu 2009
Kayes 22,190 327,891 513,362
Bafoulabé 20,220 168,731 233,926
Kéniéba 12,883 144,971 194,153
Kita 35,250 303,647 434,379
Diéma 12,440 141,905 212,062
Nioro 11,060 165,708 230,488
Yélimane 5,700 121,463 178,442

Marejeo[hariri | hariri chanzo]

  1. Communes de la Région de Kayes (PDF) (kwa Kifaransa), Ministère de l’administration territoriale et des collectivités locales, République du Mali, ilihifadhiwa kwenye nyaraka kutoka chanzo (PDF) mnamo 2012-09-19.