Mkoa wa Taoudenit

Kutoka Wikipedia, kamusi elezo huru
Maeneo ya Taoudenit (nyekundu)
Ramani hii inaonyesha Taoudenit kama sehemu ya Mkoa wa Timbuktu

Taoudénit (kwa Kibambara: Taudeni Dineja) ni mkoa wa Mali ulioundwa kisheria mwaka wa 2012 kutoka sehemu ya kaskazini ya Mkoa wa Timbuktu. [1] [2]

Utekelezaji halisi wa uanzishwaji wa mkoa huo ulianza tarehe 19 Januari 2016 kwa kumteua Abdoulaye Alkadi kuwa gavana wa eneo hilo. [3] Wajumbe wa baraza la mpito la mkoa waliteuliwa tarehe 14 Oktoba 2016. [4] Jenerali Abderrahmane Ould Meydou alichukua nafasi ya Alkadi kama gavana mnamo Julai 2017. [5]

Mkoa umegawanywa katika wilaya (cercles) sita: Achouratt, Al-Ourche, Araouane, Boudje-Beha, Foum-Alba na Taoudenit. [6] Makao makuu yanapangwa kuwa Taoudenit, [6] ingawa serikali kwa sasa iko Timbuktu kutokana na ukosefu wa miundombinu huko Taoudenit [7], pamoja na hali tata ya usalama.

Marejeo[hariri | hariri chanzo]

  1. LOI No 2012-017 DU 02 MARS 2012 PORTANT CREATION DE CIRCONSCRIPTIONS ADMINISTRATIVES EN REPUBLIQUE DU MALI. Journal officiel de la République du Mali (2 March 2012). Jalada kutoka ya awali juu ya 2018-11-23. Iliwekwa mnamo 21 February 2017.
  2. Report of the Secretary-General on the situation in Mali. MINUSMA (28 March 2016). Iliwekwa mnamo 21 February 2017.
  3. Régionalisation: Deux Nouvelles régions créées au Mali. Malijet (21 January 2016). Jalada kutoka ya awali juu ya 2017-02-22. Iliwekwa mnamo 21 February 2017.
  4. Report of the Secretary-General on the situation in Mali, Tovuti ya Minusma tar. 30.12.2016
  5. Taoudenit : Le général Ould Meydou installé dans ses fonctions de gouverneur de région. Malizine (22 July 2017). Iliwekwa mnamo 18 October 2018.
  6. 6.0 6.1 Mali : Taoudeni, contrée historique (21 February 2017). Jalada kutoka ya awali juu ya 2022-01-10. Iliwekwa mnamo 25 May 2017.
  7. Report of the Secretary-General on the situation in Mali. MINUSMA (30 December 2016). Iliwekwa mnamo 21 February 2017."Report of the Secretary-General on the situation in Mali" (PDF). MINUSMA. 30 December 2016. Retrieved 21 February 2017.