Majimbo ya Sudan Kusini

Majimbo ya Sudan Kusini ni vitengo vya Jamhuri ya Sudan Kusini yenye madaraka ya kujitawala kulingana na katiba ya nchi. Kila jimbo huwa na bunge na serikali yake inayoongozwa na gavana.
Idadi ya majimbo ni 10. Majimbo hayo yaliundwa kutoka kwa majimbo matatu ya kihistoria ya zamani (ambayo ni pia kanda za kisasa) ya Bahr el Ghazal (kaskazini-magharibi), Equatoria (kusini), na Greater Upper Nile (kaskazini mashariki). Majimbo hayo yamegawanywa zaidi katika wilaya (counties) 79 .
Mnamo Oktoba 2015, Rais wa Sudan Kusini Salva Kiir Mayardit alitangaza kugawa majimbo hayo 10 kuwa 28. Mwezi Novemba 2015 bunge la Sudan Kusini liliidhinisha kuundwa kwa majimbo mapya. Mnamo Januari 2017, Rais Salva Kiir alitangaza amri ya kuongeza tena idadi ya majimbo kutoka 28 hadi majimbo 32. [1]
Lakini kwenye Februari 2020 nchi ilirejea katika majimbo 10 ya awali pamoja na maeneo mawili ya kiutawala, Pibor na Ruweng, na eneo la hali maalum ya kiutawala la Abyei . [2] [3] Mabadiliko hayo yalikuwa tokeo la makubaliano ya amani yaliyomaliza Vita ya wenyewe kwa wenyewe ya Sudan Kusini,
Eneo la Abyei linachukuliwa kuwa sehemu ya Jamhuri ya Sudan na Jamhuri ya Sudan Kusini kwa wakati mmoja. Eneo la Kafia Kingi linazaniwa kati ya Sudan Kusini na Sudan na Pembetatu ya Ilemi inazaniwa kati ya Sudan Kusini na Kenya.
Majimbo kumi na maeneo matatu (2020-sasa)
Marejeo
- ↑ South Sudanese President creates four more states – Sudan Tribune: Plural news and views on Sudan (en). www.sudantribune.com. Jalada kutoka ya awali juu ya 2017-09-18. Iliwekwa mnamo 1 March 2017.
- ↑ South Sudan Kiir agrees to re-establish the 10 states - Sudan Tribune: Plural news and views on Sudan. www.sudantribune.com. Jalada kutoka ya awali juu ya 2020-11-01. Iliwekwa mnamo 15 February 2020.
- ↑ Kiir agrees to relinquish controversial 32 states (en). Radio Tamazuj. Iliwekwa mnamo 15 February 2020.
- ↑ 4.0 4.1 Statistical Yearbook for Southern Sudan 2010. Southern Sudan Centre for Census, Statistics and Evaluation. Jalada kutoka ya awali juu ya 2012-10-18. Iliwekwa mnamo 2023-03-19.
- ↑ Kiir fires Warrap governor, appoints a successor (en).
- ↑ Budhok Ayang Kur appointed Governor of Upper Nile state (en) (29 January 2021). Jalada kutoka ya awali juu ya 2022-12-08. Iliwekwa mnamo 2023-03-19.
- ↑ New Pibor chief administrator vows to restore peace, security (en).
- ↑ South Sudan's Kiir sacks Ruweng chief administrator (June 6, 2022). Jalada kutoka ya awali juu ya 2022-06-09. Iliwekwa mnamo 2023-03-19.