Mikoa ya Jamhuri ya Kongo

Kutoka Wikipedia, kamusi elezo huru
Mikoa ya Jamhuri ya Kongo.

Mikoa ya Jamhuri ya Kongo ni ngazi ya kwanza ya ugatuzi wa utawala katika Jamhuri ya Kongo. Nchi imegawanywa katika mikoa kumi na mbili zinazoitwa kwa Kifaransa départements tangu mwaka 2002. [1]

Mikoa hiyo imegawanywa katika wilaya 86 na halmashauri 7. Hizo zimegawanywa zaidi katika jumuiya za mjini (communautés urbaines) na jumuiya za vijijini (communautés rurales); ambazo zimegawanywa zaidi katika mitaa (quartiers) na vijiji.

Mkoa Makao makuu Idadi ya watu
(sensa ya 2007)
Eneo
(km2)
Kanda
Kouilou Hinda 91,955 13,650 Kusini
Niari Dolisie 231,271 25,942 Kusini
Lekoumou Sibiti 96,393 20,950 Kusini
Bouenza Madingou 309,063 12,265 Kusini
Pool Kinkala 236,595 33,955 Kusini
Plateaux Djambala 174,591 38,400 Kaskazini
Cuvette Owando 156,044 48,250 Kaskazini
Cuvette-Ouest Ewo 72,999 26,600 Kaskazini
Sangha Ouesso 85,738 55,800 Kaskazini
Likouala Impfondo 154,155 66,044 Kaskazini
Brazzaville 1,373,382 100 Kusini
Pointe-Noire 715,335 44 Kusini

Marejeo[hariri | hariri chanzo]

  1. "Statoid site page on the Congo with additional sources listed". Statoids.com. Iliwekwa mnamo 2012-04-22. 

Viungo vya nje[hariri | hariri chanzo]

Makala hii kuhusu maeneo ya Afrika bado ni mbegu.
Je unajua kitu kuhusu Mikoa ya Jamhuri ya Kongo kama historia yake, biashara, taasisi zilizopo, watu au utamaduni?
Labda unaona habari katika wikipedia ya Kiingereza au lugha nyingine zinazofaa kutafsiriwa?
Basi unaweza kuisaidia Wikipedia kwa kuihariri na kuongeza habari.