Nenda kwa yaliyomo

Mkoa wa Dakar

Kutoka Wikipedia, kamusi elezo huru
Mkoa wa Dakar (Senegal) na wilaya zake

Mkoa wa Dakar (kwa Kifar.: Region de Dakar) ni mkoa mdogo kabisa kati ya mikoa 14 ya Senegal lakini ni mkoa wa mji mkuu na pia mkoa wenye wakazi wengi.

Mkoa huo unajumlisha mji mkuu Dakar, pamoja na miji ya karibu Pikine, Guédiawaye na Rufisque kwenye rasi ya Cap-Vert ambayo ni sehemu ya Afrika bara iliyopo upande wa magharibi zaidi.

Mkoa wa Dakar umegawanywa katika wilaya (departements) nne.

Wilaya Eneo (km 2 ) Idadi ya watu
Sensa ya 2013
Dakar 79 1,146,053
Guédiawaye 13 329,659
Pikine 87 1,170,791
Rufisque 372 490,694
Jumla ya Mkoa wa Dakar 547 3,137,196

Viungo vya nje[hariri | hariri chanzo]