Mfumo wa jua

Kutoka Wikipedia, kamusi elezo huru
(Elekezwa kutoka Mfumo wa jua na sayari zake)
Rukia: urambazaji, tafuta
Jua letu na sayari zake.
Sayari nne kubwa ziliundwa hasa na gesi, nyingine ni sayari ndogo kama dunia yetu za mwamba.[1]

Mfumo wa jua (ing. solar system) ni utaratibu wa jua letu, sayari na sayari kibete zinazolizunguka pamoja na miezi yao, asteroidi, meteoridi, kometi na vumbi ya angani, vyote vikishikwa na mvutano wa jua.

Utaalamu kuhusu mfumo wa jua hujadiliwa katika fani ya astronomia.

Kwa kawaida siku hizi, baada ya kutambua Pluto kama sayari kibete, huhesabiwa sayari nane zinazozunguka jua. Lakini miaka ya nyuma magimba makubwa yamegunduliwa angani ambayo bado hayajakubaliwa kama yahesabiwe kuwa sayari au aina ya asteoridi.

Orodha inayofuata bado inahitaji kuangaliwa kwa sababu kuna tofauti kati ya kamusi na vitabu mbalimbali jinsi ya kutaja sayari fulani.

Sayari za jua letu[hariri | hariri chanzo]

Sayari ambazo zipo katika mfumo wa jua ni kama zifuatazo:

Namba zote zinazotaja sifa mbalimbali za sayari zinaonyesha kipimo kulingana na tabia za dunia yetu kuwa "1". Kuhusu majina ya sayari kadhaa kuna mchanganyiko katika kamusi na vitabu. Pale ambako jina au umbo tofauti la jina ni la kawaida linaonyeshwa katika mabano kama (jina). Majina yanayotumiwa katika vitabu kadhaa, hasa vya shule za msingi, bila kuwa na uhakika yanaonyeshwa katika mabano ya italiki pamoja na alama ya swali kama (? jina). [2]

* Utaridi ni jina la sayari ya kwanza kutokana na lugha ya Kiarabu na pia katika mapokeo ya Kiswahili tangu kale. Vitabu vingine hutumia neno "Zebaki" ambalo pia lina asili ya Kiarabu likimaanisha metali mojawapo; inaonekana limepatikana kama tafsiri ya jina la Kiingereza la sayari ya kwanza "Mercury" bila kujua historia ya majina ya sayari sita ya kwanza yaliyoingia katika Kiswahili kutoka lugha ya Kiarabu. [3]
** Zuhura - Ng'andu ni sayari ambalo kwa Kiswahili lina jina la Kibantu pamoja na jina lenye asili ya Kiarabu
*** Tazama makala ya Dunia kwa ajili ya namba halisi. Neno "ardhi" hutumika na waandishi kadhaa badala ya "dunia" wakitaka kutaja sayari ya tatu.
**** Tangu mwaka 2006 Pluto imeingizwa katika kundi la "sayari kibete" Katika vitabu vya shule ya msingi inatajwa mara nyingi kwa jina Utaridi - ambayo haiwezekani maana Pluto haikujulikana kabla ya mwaka 1931 lakini "Utaridi" ni jina linalopatikana tangu zamani kwa Kiswahili likimaanisha sayari ya kwanza.
Jina la sayari Kipenyo kwenye ikweta
kulingana na kipenyo cha dunia = 1
Masi Nusukipenyo ya mzingo wa kuzunguka jua Muda wa mzingo
(miaka)
Kuinama kwa mzingo wa kuzunguka jua
Pembenukta (°)
Muda wa siku ya sayari
(siku)
Miezi
Utaridi
(? Zebaki)*
0.382 0.06 0.387 0.241  7.00 58.6 0
Zuhura (Ng'andu)** 0.949 0.82 0.72 0.615  3.39 -243 0
Dunia (Ardhi)*** 1.00 1.00 1.00 1.00  0.00 1.00 1
Mirihi (Murihi, Meriki, Mars) 0.53 0.11 1.52 1.88  1.85 1.03 2
Mshtarii
(? Sumbula)
11.2 318 5.20 11.86  1.31 0.414 63
Zohari (Zohali, pia Zuhali)
(? Sarateni)
9.41 95 9.54 29.46  2.48 0.426 49
Uranus
(? Zohali)(? Sarteni)
3.98 14.6 19.22 84.01  0.77 -0.718 27
Neptun
(Kausi)
3.81 17.2 30.06 164.8  1.77 0.671 13
Pluto
(? Utaridi)****
0.18 0.002 39.5 248.5 17.1     -6.5 3

Sayari za nyongeza?[hariri | hariri chanzo]

Katika miaka iliyopita wanaastronomia wamejadili uwezekano wa kuwepo kwa sayari za ziada katika umbali mkubwa. Imetambuliwa ya kwamba muundo wa mfumo wa jua ni kubwa kuliko wataalamu wa kale walifikiri.

Tangu kutambuliwa wa ukanda wa Kuiper ambamo Pluto ni sehemu tu inajulikana ya kwamba kuna magimba ya angani mengi yasiyoonekana kwa kirahisi kwa sababu yanapokea na kuakisia nuru kidogo sana kutoka jua.

Kuhusu magimba ya angani yaliyombali zaidi kuliko ukanda wa Kuiper hakuna uhakika bado, Lakini tangu mwaka 2012 vipimo vyipya vilisababisha kutokea kwa nadharia tele kuhusu sayari ya tisa katika umbali mkubwa sana ambyo haikutazamiwa bado.

Mfumo wa jiosentriki[hariri | hariri chanzo]

Ulikuwa mfumo wa sayari, jua, nyota na magimba mengine angani ambao zamani ulipendekeza kwamba vyote vinazunguka dunia, ambayo ndiyo ilichukuliwa kuwa kitovu cha ulimwengu.

Marejeo[hariri | hariri chanzo]

  1. Hand, Eric (January 20, 2016).
  2. Linganisha ukurasa wa majadiliano:sayari
  3. kuhusu majina ya sayari zilizojulikana kwa Waswahili na hivyo kuwa na majina asilia, linganisha Jan Knappert, Swahili Islamic poetry, Brill 1971, Vol 1 uk 96-97 - taz google booksearch [1]
Science-symbol-2.svg Makala hii kuhusu mambo ya sayansi bado ni mbegu.
Je, unajua kitu kuhusu Mfumo wa jua kama historia yake au mahusiano yake na mada nyingine?
Labda unaona habari katika Wikipedia ya Kiingereza au lugha nyingine zinazofaa kutafsiriwa?
Basi unaweza kuisaidia Wikipedia kwa kuihariri na kuongeza habari.