Lazaro wa Bethania

Lazaro (kwa Kiebrania אלעזר, Eleazar au Eliezer) ni mtu anayetajwa katika Injili ya Yohane: aliishi katika karne ya 1 huko Bethania, kijiji karibu na Yerusalemu, pamoja na dada zake Martha na Maria.
Yesu Kristo alifurahia urafiki wao wote, hasa alipokuwa akihiji kwenda Yerusalemu.
Katika nafasi ya mwisho ya kufanya hivyo, alimfufua siku ya nne baada ya kifo chake, jambo lililofanya wengi wamuamini kuwa ndiye Kristo, lakini pia wapinzani wake waharakishe kifo chake mwenyewe.
Lazaro anaheshimiwa na Kanisa Katoliki, na Waorthodoksi na wengineo kama mtakatifu.
Sikukuu yake huadhimishwa tarehe 29 Julai[1].
Michoro ya Ufufuko wa Lazaro[hariri | hariri chanzo]
File:Lazarus, Russian icon.jpg|Ufufuko wa Lazaro, picha takatifu ya Kirusi, karne ya 15, kazi ya Shule ya Novgorod; iko (State Russian Museum, Saint Petersburg) File:Sebastiano del Piombo, The Raising of Lazarus.jpg|Ufufuko wa Lazaro, mchoro wa miaka 1517-1519, kazi ya Sebastiano del Piombo (National Gallery, London) File:Michelangelo Caravaggio 006.jpg|Ufufuko wa Lazaro]], mchoro wa mwaka 1609 hivi, kazi ya Michelangelo Merisi da Caravaggio (Museo Regionale, Messina) File:Rembrandt Harmensz. van Rijn 015.jpg|Ufufuko wa Lazaro, 1630-1631, mchoro wa Rembrandt van Rijn (Los Angeles County Museum of Art, Los Angeles) File:Giuseppe salviati, resurrezione di lazzaro.jpg|Ufufuko wa Lazaro, 1540-1545, mchoro wa Rembrandt van Rijn File:Vincent Van Gogh- La Résurrection de Lazare (d’après Rembrandt).JPG|Ufufuko wa Lazaro (kufuatana na Rembrandt), 1890, mchoro wa Vincent van Gogh (Van Gogh Museum, Amsterdam) File:Bonnat01.jpg|Ufufuko wa Lazaro, 1857, mchoro wa Léon Joseph Florentin Bonnat </gallery>
Tazama pia[hariri | hariri chanzo]
- Watakatifu wa Agano la Kale
- Orodha ya Watakatifu Wakristo
- Orodha ya Watakatifu wa Afrika
- Orodha ya Watakatifu Wafransisko
- Miujiza ya Yesu
Tanbihi[hariri | hariri chanzo]
Viungo vya nje[hariri | hariri chanzo]
![]() |
Makala hii bado ni mbegu. Je, unajua kitu kuhusu Mkristo huyu, kama wasifu wake, habari za maisha au kazi yake? Je, unaona habari katika Wikipedia ya Kiingereza au lugha nyingine zinazofaa kutafsiriwa? Basi unaweza kuisaidia Wikipedia kwa kuihariri na kuiongezea habari. |