Nenda kwa yaliyomo

Martha wa Bethania

Kutoka Wikipedia, kamusi elezo huru
Kristo nyumbani mwa Martha na Maria kadiri ya mchoro wa Johannes Vermeer (1654 hivi) unaotunzwa kwenye National Gallery of Scotland, Edinburgh. Martha amesimama karibu na Yesu.
Mfululizo wa kurasa juu ya Yesu
Yesu
Yesu Kristo na Ukristo

Umwilisho   Utoto wa Yesu   Ubatizo   Arusi ya Kana   Utume wa Yesu   Mifano ya Yesu   Miujiza ya Yesu   Kugeuka sura   Karamu ya mwisho   Msalaba wa Yesu   Maneno saba   Kifo cha Yesu   Ufufuko wa Yesu   Kupaa mbinguni   Ujio wa pili  Yesu na matabiri ya Agano la Kale   Injili   Majina ya Yesu katika Agano Jipya   Yesu kadiri ya historia   Tarehe za maisha ya Yesu   Kristolojia

Mazingira ya Yesu

Wayahudi   Kiaramu   Bikira Maria   Yosefu (mume wa Maria)   Familia takatifu   Ukoo wa Yesu   Ndugu wa Yesu   Yohane Mbatizaji

Mitazamo juu ya Yesu

Mitazamo katika Agano Jipya  · Mitazamo ya Kikristo   Mitazamo ya Kiyahudi   Mitazamo ya Kiislamu   Yesu katika sanaa

Martha wa Bethania (jina lake kwa Kiebrania na Kiaramu ni מַרְתָּא, Martâ, kwa Kigiriki Μαρθα, Martha) alikuwa mwanamke wa Bethania, kitongoji cha Yerusalemu, katika karne ya 1[1].

Ndugu zake walikuwa Maria na Lazaro wa Bethania, ambao wote Yesu alifurahia urafiki wao alipokuwa akihiji kwenda Yerusalemu.

Wanaheshimiwa na Wakristo wengi kama watakatifu[2].

Sikukuu yao inaadhimishwa pamoja tarehe 29 Julai[3] au 4 Juni, kadiri ya madhehebu.

Anajulikana hasa kutokana na Injili, kwa namna ya pekee Injili ya Luka (10:38-42)[4] na Injili ya Yohane (11), katika Agano Jipya ndani ya Biblia ya Kikristo.

Humo anaonekana mwenye silika ya utendaji na imani kwa Yesu Kristo, ambaye alipendezwa na ukarimu wake, pamoja na kumuonya azingatie kwanza kilicho muhimu pekee, yaani kusikiliza Neno la Mungu.

Kisha kumkiri Yesu kuwa Kristo, Mwana wa Mungu aliyekuja ulimwenguni, alishuhudia alivyomfufua kaka yake Lazaro siku nne baada ya kifo chake.

Maneno yake kwa Yesu yalikuwa haya: "Bwana, kama ungalikuwapo hapa, ndugu yangu hangalikufa. Lakini hata sasa najua ya kuwa yoyote utakayomwomba Mungu, Mungu atakupa... Naam, Bwana, mimi nimesadiki ya kwamba wewe ndiwe Kristo, Mwana wa Mungu, yule ajaye ulimwenguni". (Yoh. 11:21-22, 27)

Tazama pia

[hariri | hariri chanzo]
  1. https://www.santiebeati.it/dettaglio/23750
  2. https://www.santiebeati.it/dettaglio/99081
  3. Martyrologium Romanum
  4. Masomo ya Breviari - Sikukuu za Bwana, za Bikira Maria na za Watakatifu - Ndanda Mission Press 1978, uk 251-253

Marejeo ya Kiswahili

[hariri | hariri chanzo]
  • John Kabeya na wengine - Maisha ya Watakatifu – ed. T.M.P. Book Department – Tabora 1965, 1989, uk. 259-260
  • Pd. Leandry Kimario, O.F.M.Cap. - Mfahamu Mtakatifu Somo Wako - Maisha ya Watakatifu wa Kila Siku pamoja na Watakatifu Wafransisko - Toleo la pili - Dar es Salaam 2021, uk. 218-219
  • Maurice Soseleje, Kalendari yetu – Maisha ya Watakatifu – Toleo la pili – ed. Benedictine Publications Ndanda Peramiho – Peramiho 1986 – ISBN 9976-63-112-X, uk. 60

Viungo vya nje

[hariri | hariri chanzo]
Wikimedia Commons ina media kuhusu:
  • "St. Martha, Virgin", Butler's Lives of the Saints
  • St. Martha on catholic.org
  • Mary & Martha, the sisters of Lazarus Ilihifadhiwa 26 Oktoba 2009 kwenye Wayback Machine., Greek Orthodox Archdiocese of America
  • Patron Saints: Martha Ilihifadhiwa 29 Septemba 2007 kwenye Wayback Machine.
  •  "St. Martha" . Catholic Encyclopedia. New York: Robert Appleton Company. 1913.
  • "The Life of Saint Martha" Ilihifadhiwa 30 Machi 2010 kwenye Wayback Machine., text from the Golden Legend
Makala hii kuhusu mtu wa Biblia bado ni mbegu.
Je, unajua kitu kuhusu Martha wa Bethania kama habari za maisha au kazi yake?
Labda unaona habari katika Wikipedia ya Kiingereza au lugha nyingine zinazofaa kutafsiriwa?
Basi unaweza kuisaidia Wikipedia kwa kuihariri na kuongeza habari.