Nenda kwa yaliyomo

Maria wa Bethania

Kutoka Wikipedia, kamusi elezo huru
Kristo nyumbani mwa Martha na Maria kadiri ya mchoro wa Johannes Vermeer (1654 hivi) unaotunzwa kwenye National Gallery of Scotland, Edinburgh. Maria ameketi miguuni pa Yesu.
Mfululizo wa kurasa juu ya Yesu
Yesu
Yesu Kristo na Ukristo

Umwilisho   Utoto wa Yesu   Ubatizo   Arusi ya Kana   Utume wa Yesu   Mifano ya Yesu   Miujiza ya Yesu   Kugeuka sura   Karamu ya mwisho   Msalaba wa Yesu   Maneno saba   Kifo cha Yesu   Ufufuko wa Yesu   Kupaa mbinguni   Ujio wa pili  Yesu na matabiri ya Agano la Kale   Injili   Majina ya Yesu katika Agano Jipya   Yesu kadiri ya historia   Tarehe za maisha ya Yesu   Kristolojia

Mazingira ya Yesu

Wayahudi   Kiaramu   Bikira Maria   Yosefu (mume wa Maria)   Familia takatifu   Ukoo wa Yesu   Ndugu wa Yesu   Yohane Mbatizaji

Mitazamo juu ya Yesu

Mitazamo katika Agano Jipya  · Mitazamo ya Kikristo   Mitazamo ya Kiyahudi   Mitazamo ya Kiislamu   Yesu katika sanaa

Maria wa Bethania (jina lake kwa Kiebrania מִרְיָם, Miryām, kwa Kiaramu מרים, Maryām, kwa Kigiriki Μαρία, Maria) alikuwa mwanamke wa Bethania, kitongoji cha Yerusalemu, katika karne ya 1[1].

Ndugu zake walikuwa Martha na Lazaro wa Bethania, ambao wote Yesu alifurahia urafiki wao hasa alipohiji kwenda Yerusalemu.

Wanaheshimiwa na Wakristo wengi kama watakatifu[2].

Sikukuu yao inaadhimishwa pamoja tarehe 29 Julai[3] au 4 Juni, kadiri ya madhehebu.

Anajulikana hasa kutokana na Injili, kwa namna ya pekee Injili ya Luka (10:38-42)[4] na Injili ya Yohane (11; 12:1-8), katika Agano Jipya ndani ya Biblia ya Kikristo.

Humo anaonekana mwenye silika ya utulivu na imani kwa Yesu Kristo, ambaye alipendezwa sana na usikivu wake wakati alimfundisha ameketi chini karibu na miguu yake, kama ilivyokuwa kawaida ya wanafunzi wa dini ya Kiyahudi, ingawa wakati huo wanaume tu walikubalika.

Tazama pia

[hariri | hariri chanzo]
  1. https://www.santiebeati.it/dettaglio/96761
  2. https://www.santiebeati.it/dettaglio/99081
  3. Martyrologium Romanum
  4. Masomo ya Breviari - Sikukuu za Bwana, za Bikira Maria na za Watakatifu - Ndanda Mission Press 1978, uk 251-253

Viungo vya nje

[hariri | hariri chanzo]
Makala hii kuhusu mtu wa Biblia bado ni mbegu.
Je, unajua kitu kuhusu Maria wa Bethania kama habari za maisha au kazi yake?
Labda unaona habari katika Wikipedia ya Kiingereza au lugha nyingine zinazofaa kutafsiriwa?
Basi unaweza kuisaidia Wikipedia kwa kuihariri na kuongeza habari.