Nenda kwa yaliyomo

Utoaji mimba

Kutoka Wikipedia, kamusi elezo huru
(Elekezwa kutoka Kutoa mimba)
Mimba ya wiki 10 hivi iliyotolewa tumboni mwa mama kwa njia ya upasuaji.

Utoaji mimba au Uavyaji wa mimba ni tendo la hiari la kuua mimba iliyokwishatungwa tumboni mwa mwanamke. Unaweza kufanywa naye au na watu wengine kwa kibali chake au bila ya hicho.

Sababu zinaweza kuwa mbalimbali: hatari kwa uhai wa mjamzito, haya kwa tendo lililotunga mimba kinyume cha maadili, hali ya uchumi, ulemavu wa mama au wa mimba, ubaguzi wa jinsia n.k.

Ni tofauti na tukio lisilokusudiwa la mimba kuharibika kwa sababu mbalimbali.

Mbinu zake

[hariri | hariri chanzo]

Mimba inaweza ikatolewa kwa hiari kwa njia nyingi. Namna iliyochaguliwa hutegemea hasa umri wa kiinitete au kijusi, ambacho hukua kwa ukubwa kadiri siku zinavyopita. [1]

Mbinu inaweza ikachaguliwa kulingana na uhalalisho wa utoaji mimba, upatikanaji, na uamuzi wa daktari na mjamzito.

Kwa kutumia dawa

[hariri | hariri chanzo]

Utoaji mimba ambao unatumia dawa huchangia 10% ya utoaji mimba wote huko Marekani na Ulaya.

Iwapo itashindikana kutoa mimba kwa njia hiyo, usafishaji wa ombwe au uondoaji kwa mikono hutumika[2].

Upasuaji

[hariri | hariri chanzo]

Katika wiki 12 za kwanza, ufyonzaji au kuavya kwa uvutaji ombwe ndiyo mbinu inayotumika sana.

Utanuaji na ukwanguaji ni njia ya pili inayotumiwa sana katika uavyaji mimba, ni utaratibu wa wastani wa kiginakolojia unaofanywa kwa sababu mbalimbali, ikiwa ni pamoja na uchunguzi wa uvimbe wowote hatari katika ukuta wa mfuko wa uzazi, uchunguzi wa utokaji damu usiokuwa wa kawaida na utoaji wa mimba.

Mbinu nyingine lazima zitumike tu kuavya mimba katika miezi mitatu ya pili ya ujauzito. Uzazi wa kabla ya kipindi kuwadia unaweza kuchochewa kwa kutumia dawa zinazotoa mimba; hii inaweza kuambatanishwa na kudungwa sindano iliyo na mchanganyiko wa toni ya misuli (haipatoni) pamoja na chumvi au urea kwenye majimaji ya amnioni.

Baada ya wiki 16 za ujauzito, uavyaji mimba unaweza kusababishwa kwa utanuaji na uchopoaji kamili, yaani ugandamuaji wa fuvu la kichwa kizazini, ambao huhitaji ugandamuaji wa fuvu la kichwa cha kijusi kabla ya kuchopolewa. Wakati mwingine huitwa "uzazi mdogo wa utoaji mimba", ambao umepigwa marufuku nchini Marekani.

Utoaji mimba kwa njia ya histerotomia ni utaratibu sawa na upasuaji wa sehemu na unafanya kazi chini ya dawa ya usingizi wa ujumla. Huhitaji upasuaji mdogo ukilinganishwa na upasuaji mkubwa na hutumika ujauzito ukiwa kwenye hatua za mwisho.

Kutoka wiki ya 20 mpaka ya 23 ya umri wa mimba, sindano ya kuzuia moyo wa kichanga inaweza ikatumika kama awamu ya kwanza ya utoaji mimba kwa taratibu za kiupasuaji[3][4] [5] [6] [7] [8] na kuhakikisha kwamba kijusi si kizaliwa hai. [9]

Njia nyinginezo

[hariri | hariri chanzo]

Kihistoria, idadi ya mimea inayosadikika kuna na uwezo wa kutoa mimba zimetumika katika utabibu wa asili: tansia, penniroyali, kohoshi mweusi, na silifiamu iliyopo sasa. [10] Matumizi ya mitishamba kwa namna fulani yanaweza kusababisha hata madhara yaletayo kifo, kama vile kushindwa kwa viungo mbalimbali vya mwili, na hazipendekezwi na daktari. [11]

Utoaji mimba wakati mwingine ni kujaribu na kusababisha athari ya maumivu ya tumbo. Kiwango cha nguvu, kikiwa kikali, kinaweza kusababisha majeraha makubwa ndani bila ya ulazima wa mimba kutoka.

Katika Asia ya Kusini, kuna mapokeo ya kujaribu kutoa mimba kwa kuchua tumbo kwa nguvu. Moja ya mabango ya michoro ya mapambo ya hekalu la Angkor Wat katika Cambodia linaonyesha pepo likifanya utoaji mimba kwa mwanamke ambaye alimtuma kutoka kuzimu.

Mbinu nyingine iliyoripotiwa ya utoaji mimba wa kujitegemea ni pamoja na matumizi mabaya ya dawa inayofanana na vichocheo vya mwili yaani misoprostoli, na uingizaji wa vifaa visivyo vya kiupasuaji kama sindano za kufumia na kiango cha nguo ndani ya mji wa mimba.

Utoaji mimba na uzazi wa mpango

[hariri | hariri chanzo]

Utoaji mimba unaweza kuwa chini ya dhima ya makosa ya jinai katika nchi mbalimbali. Lakini siku hizi katika nchi nyingi utoaji mimba umehalalishwa na mabunge na umekuwa ukichangiwa na serikali.

Kwa njia hiyo kila mwaka watoto milioni mia na zaidi wanaangamizwa kwa ukatili wasizaliwe, bila ya kuhesabu wale wanaouawa na vidonge, sindano, poda, vitanzi na vipandikizi, pengine bila ya wahusika kujua wala kutambua kilichotokea, kwa kuwa hivyo vinatangazwa kama njia za uzazi wa mpango unaoratibu upatikanaji wa mimba, kumbe ukweli ni kwamba vinaua mimba zilizokwishaumbwa, mbali ya kwamba vinaharibu afya ya akina mama.

Kuna pia njia nyingine za kuzuia uzazi, kama vile: kumwaga mbegu nje ya tumbo la uzazi, kuvaa mipira ya kiume na ya kike, kufunga kizazi cha mwanamume au cha mwanamke: ingawa njia hizo haziui mimba, zinaleta madhara kwa wanaozifuata, tena zinashindikana kwa kiasi tofauti. Hapo mtu aliyekusudia kukwepa mimba kwa mbinu yoyote anafikia kwa urahisi fulani uamuzi wa kuiua: hivyo hata njia hizo zinaweza zikaandaa njia kwa mauaji ya halaiki.

Mjadala kuhusu uhalali wake

[hariri | hariri chanzo]

Katika historia utoaji mimba umekuwa chanzo cha mjadala mkubwa unaotatanisha miongoni mwa wanaharakati. Msimamo wa mtu kuhusu suala hilo na mengine tata upande wa maadili, falsafa, biolojia na sheria, mara nyingi huhusiana na mfumo wa maadili wa mtu huyo.

Misimamo mikuu ni kati ya wanaodai haki ya kuchagua, msimamo unaotetea uavyaji mimba, na watetea uhai, msimamo unaopinga uavyaji mimba.

Maoni kuhusu utoaji mimba yanaweza kuelezewa kama mseto wa imani kuhusu uadilifu wake, kuhusu uwajibikaji, na kiwango sahihi cha mamlaka ya serikali katika kutunga sera za umma.

Maadili ya dini pia yana ushawishi katika maoni ya mtu binafsi na mjadala mzima kuhusu uavyaji.

Mijadala kuhusu uavyaji mimba, hasa sheria zinazohusu uavyaji, mara nyingi huongozwa na makundi ya kutetea moja ya pande hizi mbili.

Kwa jumla, msimamo wa watetea uhai ni kuwa kijusi cha binadamu ni binadamu aliye na haki ya kuishi hivyo kuavya mimba ni sawa na uuaji. Msimamo wa wanaodai uhuru wa kuchagua ni kuwa mwanamke ana kiwango fulani cha haki kuhusu tumbo la uzazi hata kuchagua ikiwa atabeba mimba kwa muda wote au la.

Mjadala pia huangazia ikiwa mwanamke mjamzito anapaswa kuwaarifu / au kupata ridhaa ya watu wengine katika uamuzi huo: ikiwa nimtoto aulize wazazi wake; ikiwa ni mke wa mtu amuambie mumewe; au mwanamke mjamzito amuambie aliyempa mimba.

Mtazamo wa dini

[hariri | hariri chanzo]

Dini mbalimbali zinapinga vikali tendo hilo, na Biblia inasema uuaji wa wasio na hatia unamlilia Mungu alipe kisasi.

Badala ya kuheshimu kwa shukrani maajabu ya Mungu katika uumbaji, mara nyingi binadamu aliyeshirikishwa naye kazi hiyo, amejifanya muuaji wa watoto wasiozaliwa bado na wa wale waliozaliwa pia.

  1. Menikoff, Jerry. Law and Bioethics, uk. 78 (Georgetown University Press 2001): "As the fetus grows in size, however, the vacuum aspiration method becomes increasingly difficult to use."
  2. https://www.dailywire.com/news/women-misrepresenting-chemical-abortions-as-miscarriages-at-increased-risk-of-multiple-hospitalizations-study-finds?inf_contact_key=b2f1fe496482afc6fdd13ea179293a434dfbc39d7283b2cb89d5189540b69330
  3. Bhide A, Sairam S, Hollis B, Thilaganathan B (2002). "Comparison of feticide carried out by cordocentesis versus cardiac puncture". Ultrasound Obstet Gynecol. 20 (3): 230–232. doi:10.1046/j.1469-0705.2002.00797.x. PMID 12230443. {{cite journal}}: |access-date= requires |url= (help); Unknown parameter |month= ignored (help)CS1 maint: multiple names: authors list (link)
  4. Vause S, Sands J, Johnston TA, Russell S, Rimmer S (2002). "Could some fetocides be avoided by more prompt referral after diagnosis of fetal abnormality?". J Obstet Gynaecol. 22 (3): 243–245. doi:10.1080/01443610220130490. PMID 12521492. Iliwekwa mnamo 2008-12-03. {{cite journal}}: Unknown parameter |month= ignored (help)CS1 maint: multiple names: authors list (link)
  5. Dommergues M, Cahen F, Garel M, Mahieu-Caputo D, Dumez Y (2003). "Feticide during second- and third-trimester termination of pregnancy: opinions of health care professionals". Fetal. Diagn. Ther. 18 (2): 91–97. doi:10.1159/000068068. PMID 12576743. Iliwekwa mnamo 2008-12-03.{{cite journal}}: CS1 maint: multiple names: authors list (link)
  6. Bhide A, Sairam S, Hollis B, Thilaganathan B (2002). "Comparison of feticide carried out by cordocentesis versus cardiac puncture". Ultrasound Obstet Gynecol. 20 (3): 230–232. doi:10.1046/j.1469-0705.2002.00797.x. PMID 12230443. {{cite journal}}: |access-date= requires |url= (help); Unknown parameter |month= ignored (help)CS1 maint: multiple names: authors list (link)
  7. Senat MV, Fischer C, Bernard JP, Ville Y (2003). "The use of lidocaine for fetocide in late termination of pregnancy". BJOG. 110 (3): 296–300. doi:10.1046/j.1471-0528.2003.02217.x. PMID 12628271. Iliwekwa mnamo 2008-12-03. {{cite journal}}: Unknown parameter |month= ignored (help)CS1 maint: multiple names: authors list (link)
  8. Senat MV, Fischer C, Ville Y (2002). "Funipuncture for fetocide in late termination of pregnancy". Prenat. Diagn. 22 (5): 354–356. doi:10.1002/pd.290. PMID 12001185. Iliwekwa mnamo 2008-12-03. {{cite journal}}: Unknown parameter |month= ignored (help)CS1 maint: multiple names: authors list (link)
  9. Nuffield Council on Bioethics (2006). "Clinical perspectives (Continued)". Critical Case Decisions in Fetal and Neonatal Medicine: Ethical Issues. Nuffield Council on Bioethics. ISBN 1-904384-14-5. OCLC 85782378. {{cite book}}: |access-date= requires |url= (help); |archive-url= requires |url= (help); External link in |chapterurl= (help); Unknown parameter |chapterurl= ignored (|chapter-url= suggested) (help); Unknown parameter |dead-url= ignored (|url-status= suggested) (help)
  10. Riddle, John M. (1997). Eve's herbs: a history of contraception and abortion in the West. Cambridge, Massachusetts: Harvard University Press. ISBN 0-674-27024-X. OCLC 36126503.
  11. Ciganda C, Laborde A (2003). "Herbal infusions used for induced abortion". J. Toxicol. Clin. Toxicol. 41 (3): 235–239. doi:10.1081/CLT-120021104. PMID 12807304. {{cite journal}}: |access-date= requires |url= (help)