Idd el Hajj

Kutoka Wikipedia, kamusi elezo huru
Rukia: urambazaji, tafuta
Malaika Jibril ashika mkono wa Ibrahimu kabla hajamchinja bado mwanawe
(uchoraji wa Kiosmani karne ya 16/17)

Idd el Hajj (pia: eid el hajj) ni sikukuu ya Uislamu wakati wa mwezi wa Dhul Hijjah ambao ni mwezi wa Hajj.

Majina ya sikukuu[hariri | hariri chanzo]

Kati ya Waislamu duniani sikukuu hii hujulikana kwa majina mbalimbali ambayo hutafsiriwa pia kwa lugha mbalimbali kama vile:

  • Idd-al-Adhha (kar. عيد الأضح) yaani sikukuu ya sadaka
  • Idd-al-Qorban (kar. عید قربان) sikukuu ya sadaka (kwa kutumia neno tofauti ya "sadaka" katika Qurani); Kituruki: Kurban Bayramı; Kikurdi "Cejna Kûrbanê" ;
  • Idd-al-Kabir (عيد الكبير) au "sikukuu kubwa"; "Bari Eid" huko Uhindi na Pakistan; jina hili hutumiwa kwa sababu kati ya sikukuu mbili zinazoamriwa katika Qurani hii ni sikukuu kubwa zaidi.

Sadaka ya Ibrahimu[hariri | hariri chanzo]

Idd husheherekewa kama kumbukumbu ya sadaka ya Ibrahimu (Abrahamu) ambaye kufuatana na taarifa za Biblia na za Qurani alikuwa tayari ya kumchinja mwanawe kama sadaka kwa Mungu. Lakini Mungu alimzuia asimchinje akampatia kondoo badala yake. Habari zake kati Qurani ziko sura al-Hajj aya 37, katika Biblia Mwanzo 22.

Nyama ya sadaka ya Idd-al-Hajj hugawiwa kwa maskini nchini Pakistan

Ibada zake[hariri | hariri chanzo]

Sherehe huanza na sala ya idd katika msikiti. Mara nyingi hufuatwa na baraza au mkutano wa Waislamu. Katika nchi nyingu huwa na kawaida kutembelea pia makaburi ya marehemu.

Kila Mwislamu mwenye uwezo hupaswa kumchinja mnyama wa sadaka siku hiyo mara nyingi kondoo lakini kuna pia sadaka za mbuzi, ng'ombe au ngamia kufuatana na uwezo na kawaida ya nchi.

Sehemu ya nyama ya sadaka hizo hugawiwa kwa maskini wasio na uwezo. Mengine hutumiwa kwa karamu ya familia.

Tarehe za Idd[hariri | hariri chanzo]

Idd husheherekewa kati ya tarehe 10 hadi 13 ya mwezi wa Dhul Hijjah wa kalenda ya Kiislamu. Tarehe hali halisi hutegemea na kuonekana kwa hilali au mwezi mwandamu. Hapa hutokea tofauti za kila mwaka kati ya Waislamu. Kimsingi mapokeo ya kiislamu hudai kuonekana kwa mwezi kwa macho.

Tofauti za makadirio kati ya Waislamu[hariri | hariri chanzo]

Sehemu za Waislamu hukubali ya kwamba inawezekana kukadiria tarehe hii kisayansi. Lakini huko Saudia husisitizwa kuona kwa macho. Maadamu Saudia ni mahali pa miji mitakatifu ya Maka na [Madina] na Waislamu wengine hupenda kufuata kawaida ya kule. Zamani hapakuwa sana na tatizo kwa sababu kila nchi ilikuwa na azimio lake. Mitambo ya kisasa huonyesha siku hizi kama Waislamu wameshaanza kusheherekea nchi moja lakini bado nchi nyingine. Katika nchi mbalimbali hasa pale ambako Waislamu walihamia juzi tu kama Ulaya kuna tarehe tofauti kandokando kama wengine hufuata matangazo ya Uturuki yanayokadiriwa kisayansi na wengine matangazo ya Saudia yanayofuata kuonekana kwa macho. Matangazo ya Saudia yamepingwa mara nyingi kwa sababu tarehe zilitangazwa ambapo hapakuwa na uwezekano kuona hilali kisayansi.

Kubadilika kwa tarehe katika kalenda ya jua[hariri | hariri chanzo]

Katika kalenda ya Gregori ambayo ni kalenda ya kawaida tarehe za Kiislamu hubadilika kila mara kwa sababu mwaka wa kiislamu hufuata kalenda ya mwezi lakini kalenda ya kawaida hufuata jua. Kalenda ya Kiislamu ni takriban siku 11 kasoro ya kalenda ya jua. Kila mwaka tarehe ya Idd huweza kutokea kwa siku mbili tofauti za kalenda ya Gregori kwa sababu kawaida ya Uislamu hufuata kuonekana kwa mwezi kunachopatikana tofauti duniani.

Orodha inyaofuata yaonyesha tarehe rasmi za Idd-al-Hajj kwa nchi ya Saudia jinsi ilivyotangazwa hadi 2007 na halmashauri kuu ya Majlis al-Qadā’ al-A‘lā . Tarehe za miaka 2008 na kuendelea ni tarehe zinazokadiriwa kulingana na kalenda ya Kiislamu jinsi ilivyo kawaida katika nchi kama Uturuki. Tofauti zitaendelea kutokea kulingana na maelezo hapo juu kuhusu tofautiy a makadirio na kuonekana kwa hilali

Viungo vya Nje[hariri | hariri chanzo]