Nenda kwa yaliyomo

Kalenda ya jua

Kutoka Wikipedia, kamusi elezo huru
Gari la Jua lilitengenezwa kwa hekalu ya Kigermanik katika Denmark miaka 3500 iliyopita. Wazee wale waliwaza kuwa jua linavutwa kwa gari angani. Kutazama jua kulikuwa mwanzo wa kalenda.

Kalenda ya jua ni kalenda inayofuata mwendo wa jua jinsi inavyoonekana angani. Hali halisi tunaona matokeo ya mwendo wa dunia kuzunguka jua.

Katika kalenda za jua mwaka unalingana na muda wa mzunguko mmoja wa dunia kwenye mzingo wake kuzunguka jua letu. Muda kamili wa mzunguko huu ni siku 365.2425.

Kwa kawaida kalenda za jua hutumia mwaka mwenye siku 365 na kuongeza siku moja kila baada ya miaka minne au kwa utaratibu mwingine.

Historia ya Kalenda za jua[hariri | hariri chanzo]

Kalenda nyingi za asilia zilikuwa kalenda za mwezi kwa sababu mwendo wa mwezi na vipindi vyake huhesabiwa rahisi zaidi. Lakini hesabu ya miezi halisi ina hasara ya kwamba miezi hairudi kufuatana na majira. Asili ya kalenda ya jua ni utamaduni wa wakulima katika nchi zisizo karibu na ikweta.

Katika nchi zisizo karibu na ikweta kuna majira yenye tofauti kubwa kufuatana na mwendo wa jua angani. Kwa mfano kuna kipindi ambako jua halifiki kwenye kilele cha anga wakati wa mchana na muda wa mchana ni fupi. Kipindi hiki huwa na baridi na giza. Kinyume chake kuna kipindi ambako jua linaonekana masaa mengi kila siku na mchana ni mrefu. Hiki ni kipindi cha joto.


Kalenda za Jua[hariri | hariri chanzo]

Kalenda ya jua inayojulikana zaidi ni Kalenda ya Gregori iliyokuwa kalenda ya kimataifa. Inatumia pia kipindi cha "mwezi" lakini miezi hii haina uhusiano tena na mwendo wa mwezi kama gimba la angani tena.


Kalenda zifuatazo hufuata mwendo wa jua: