Ruhuhu (mto)
Appearance
Chanzo | Milima ya Kipengere, Mkoa wa Iringa, Tanzania |
Mdomo | Ziwa Nyasa, upande wa kusini ya Manda (Ludewa) |
Nchi | Tanzania |
Urefu | ~300 km |
Mto Ruhuhu ni mto wa Tanzania Kusini. Chanzo chake kiko katika milima ya Kipengere upande wa kusini wa Njombe ikielekea kwanza kusini-mashariki na baadaye magharibi inapoishia katika Ziwa Nyasa karibu na mji wa Manda.
Mwendo wake una urefu wa kilomita zaidi ya 300. Hivyo ni tawimto mrefu wa Ziwa Nyasa na kutokana na hali hii inahesabiwa kama chanzo cha mto Shire unaopeleka maji ya ziwa kwenda mto Zambezi na Bahari Hindi.
Tazama pia
[edit | edit source]- Mito ya Tanzania
- Orodha ya mito ya mkoa wa Njombe
- Orodha ya mito ya mkoa wa Ruvuma
- Maeneo ya Kihistoria ya Kitaifa ya Tanzania
Tanbihi
[edit | edit source]Viungo vya nje
[edit | edit source]Makala hii kuhusu maeneo ya Tanzania bado ni mbegu. Je unajua kitu kuhusu Ruhuhu (mto) kama historia yake, biashara, taasisi zilizopo, watu au utamaduni? Labda unaona habari katika wikipedia ya Kiingereza au lugha nyingine zinazofaa kutafsiriwa? Basi unaweza kuisaidia Wikipedia kwa kuihariri na kuongeza habari. Usitaje majina ya madiwani na viongozi au maafisa wengine wa sasa maana wanabadilika haraka mno. |