Mkoa wa Unguja Kaskazini

Kutoka Wikipedia, kamusi elezo huru
Mkoa wa Kaskazini Unguja, Tanzania
Mahali pa Kaskazini Unguja katika Tanzania

Mkoa wa Kaskazini Unguja ni moja kati ya mikoa 26 ya Tanzania. Iko Unguja kisiwani ambayo ni kisiwa kikubwa cha Jamhuri ya Watu wa Zanzibar.

Makao makuu ya mkoa uko Mkokotoni. Kuna wilaya mbili za Kaskazini Unguja 'A' na Kaskazini Unguja 'B'.

Eneo la mkoa ni 470 km² kuna wakazi 136,953 wakiwemo Kaskazini 'A' 84,348 na Kaskazini 'B' 52,605. Wengi wanajishughulisha na uvuvi na kilimo. Sehemu ya mashariki ya mkoa kuna kilimo cha karafuu. Upande wa magharibi utalii umeanza kuwa muhimu. Eneo la Ras Nungwi ni sehemu moja penye mahoteli ya watalii wa nje.

Kisiwa cha Tumbatu ni sehemu ya mkoa huu.

Miji ya mkoa ndiyo Mkokotoni, Mahonda na Gamba.

Viungo vya nje

Dira mikoani: Kaskazini Unguja

Makala hii kuhusu maeneo ya Unguja bado ni mbegu.
Je unajua kitu kuhusu Mkoa wa Unguja Kaskazini kama historia yake, biashara, taasisi zilizopo, watu au utamaduni?
Labda unaona habari katika wikipedia ya Kiingereza au lugha nyingine zinazofaa kutafsiriwa?
Basi unaweza kuisaidia Wikipedia kwa kuihariri na kuongeza habari.
Tafadhali usiingize majina ya maafisa au viongozi wa sasa maana wanabadilika mno.