Mkoa wa Singida

Kutoka Wikipedia, kamusi elezo huru
Mahali pa Mkoa wa Singida katika Tanzania

Singida iko kati ya mikoa 26 za Tanzania ikipakana na mikoa ya Arusha, Dodoma, Iringa, Mbeya, Tabora na Shinyanga.

Kuna wilaya nne za Iramba, Manyoni, Singida Vijijini and Singida Mjini. Jumla ya wakazi ni mnamo milioni moja.

Singida ni kati ya maeneo maskini zaidi ya Tanzania. Uchumi wake ni hasa ufugaji, idadi ya ng´ombe hukadiriwa kuwa mnamo milioni 1.4. Masoko hayako karibu barabara si nzuri. Kilimo si nzuri kwa sababu ya hali ya mvua. Ukame huleta njaa. Singida ni kati ya mikoa inayotegemea misaada ya chakula.

Wakazi wa wilaya za Singida mjini na kijijini ni hasa Wanyaturu. Walio wengi Iramba ndio Wanyiramba na wakiwa Wagogo wengi huko Manyoni.