Timor ya Mashariki : Tofauti kati ya masahihisho

Kutoka Wikipedia, kamusi elezo huru
Content deleted Content added
d r2.7.2) (Roboti: Imeongeza lad:Timor Oryentala
d r2.7.1) (Roboti: Imeongeza pnb:چڑھدا تیمور
Mstari 197: Mstari 197:
[[pl:Timor Wschodni]]
[[pl:Timor Wschodni]]
[[pms:Timor Est]]
[[pms:Timor Est]]
[[pnb:چڑھدا تیمور]]
[[pt:Timor-Leste]]
[[pt:Timor-Leste]]
[[qu:Anti Timur]]
[[qu:Anti Timur]]

Pitio la 04:34, 20 Mei 2012

Timor ya Mashariki


Ramani

Timor ya Mashariki ni nchi ya Asia ya kusini-mashariki kwenye kisiwa cha Timor takriban 640 km upande wa kaskazini wa Darwin ya Australia. Eneo lake ni nusu ya mashariki ya kisiwa hiki pamoja na visiwa vya Atauro na Jaco. Kuna pia eneo dogo upande wa magharibi ya Timor ndani ya eneo la Indonesia. Upande mwingine wa kisiwa cha Timor ni chini ya Indonesia pamoja na visiwa vya jirani. Eneo lote la nchi ni 14,609 km².

Mji mkuu ni Dili mwenye wakazi 150,000.

Timor ya Mashariki ni kati ya nchi maskini zaidi duniani.

Historia

Timor ilikuwa mahali pa kituo cha biashara ya Wareno tangu karne ya 16. Maeneo mengine ya visiwa vya Indonesia ya leo yalivamiwa na Waholanzi na Timor ilibaki kisiwa cha pekee chini ya utawala wa Ureno katika sehemu hii ya dunia. Katika karne ya 19 Waholanzi walifika pia Timor. Mikataba ya 1859 na 1916 zilithebitihsa ugawaji wa kisiwa. Sehemu ya magharibi ilikuwa chini ya Uholanzi na baadaye sehemu ya Indonesia, lakini sehemu ya mashariki ilibaki koloni ya Ureno.

Baada ya mapinduzi ya Ureno ya 1974 Wareno waliondoka katika Timor bila maandalizi na kutosha. Viongozi wazalendo walitangaza uhuru. Lakini siku chache baada ya tangazo hili jeshi la Indonesia lilivamia nchi ikatangazwa kuwa jimbo la Indonesia. Hali hii haikutambuliwa na Umoja wa Mataifa.

Vita kali ya msituni ilifuata kati ya wapiganaji uhuru na jeshi la Indonesia.

Mabadiliko yalipatikana mwaka 1998 baada ya rais Suharto wa Indonesia kujiuzulu na rais mpya Bacharuddin Jusuf Habibie kuwa tayari kuipa Timor ya Mashariki hali ya kujitawala ndani ya Indonesia. Karibu wananchi wote (98 %) walihudhuria katika kura ya maoni ya 30 Agosti 1999 na zaidi ya robo tatu (78,5 %) walipigia kura uhuru badala ya kuwa jimbo la kujitawala.

Baada ya kura hii jeshi la Indonesia lililipiza kisasi kwa kuua watu wengi na kuharibu nyumba lakini macho ya dunia yalitazama Timor na serikali kwa tishio la kufutwa kwa makopo ya benki ya dunia ililazimishwa kuondoa jeshi lake na kukubali kufika kwa jeshi la Umoja wa Mataifa chini ya uongozi wa Australia.

Tangu 27 Septemba 2002 Timor ya Mashariki ni nchi mwanachama wa UM.

Viungo vya nje

Nchi na maeneo ya Asia

Afghanistan | Armenia2 | Azerbaijan | Bahrain | Bangladesh | Bhutan | Brunei | China | Falme za Kiarabu | Georgia2 | Hong Kong3 | Indonesia | Iraq | Israel | Jamhuri ya China (Taiwan) | Japani | Kamboja | Kazakhstan | Kirgizia | Korea Kaskazini | Korea Kusini | Kupro2 | Kuwait | Laos | Lebanoni | Macau3 | Malaysia | Maldivi | Mongolia | Myanmar | Nepal | Omani | Pakistan | Palestina | Qatar | Saudia | Singapuri | Sri Lanka | Syria | Tajikistan | Timor ya Mashariki | Turkmenistan | Uajemi | Ufilipino | Uhindi | Urusi1 | Uthai | Uturuki1 | Uzbekistan | Vietnam | Yemen | Yordani

1. Nchi ina maeneo katika Asia na Ulaya. 2. Nchi iko Asia lakini inahesabiwa pia kati ya nchi za Ulaya kwa sababu za historia au utamaduni. 3. Eneo la pekee la China.


Makala hii kuhusu maeneo ya Asia bado ni mbegu.
Je unajua kitu kuhusu Timor ya Mashariki kama historia yake, biashara, taasisi zilizopo, watu au utamaduni?
Labda unaona habari katika wikipedia ya Kiingereza au lugha nyingine zinazofaa kutafsiriwa?
Basi unaweza kuisaidia Wikipedia kwa kuihariri na kuongeza habari.

Kigezo:Link FA