Hati ya Gelasio
Hati ya Gelasio (kwa Kilatini Decretum Gelasianum) ni andiko la Kilatini ambalo lilidhaniwa kuwa la Papa Gelasio I (492–496). Leo hii wengi wanaona mwandishi wa kwanza alikuwa Papa Damaso I, askofu wa Roma kuanzia 366 hadi 383, ila matini yaliongezwa katika karne ya 5 na ya 6.[1]
Hati hiyo ni muhimu kutokana na orodha ya vitabu vya Biblia ndani yake ambayo ni ushuhuda wa kale zaidi kuhusu vitabu vilivyokubaliwa sehemu ya maandiko matakatifu ya Wakristo.
Andiko lote jinsi linavyopatikana lina sehemu tano:
- shairi linalojumlisha mafundisho ya Damaso I kuhusu tabia za roho ndani ya Kristo halafu tabia za Kristo mwenyewe.
- orodha ya vitabu vya Biblia
- orodha ya mapatriarki na hadhi yao
- orodha ya sinodi zinazotambuliwa na mababu wa Kanisa
- orodha ya apokrifa, ambazo zinafafanuliwa kama vitabu visivyotambuliwa na Kanisa Katoliki kama Neno la Mungu.
Sehemu 1-3 zinatazamwa kama za kale zilizotokana ama na Papa Damaso I au sinodi yake katika mwaka 382. Sehemu nyingine ziliongezwa baadaye.
Tazama pia
[hariri | hariri chanzo]Tanbihi
[hariri | hariri chanzo]- ↑ Schneemelcher, Wilhelm (1963) [1959]. New Testament Apocrypha: Gospels and Related Writings. Vol. 1. Translated by Ogg, George. Philadelphia: Westminster Press. p. 46–49. LCCN 63-7492. OCLC 7531530.
Viungo vya Nje
[hariri | hariri chanzo]- The Development of the Canon" Ilihifadhiwa 14 Mei 2011 kwenye Wayback Machine.: Decretum Gelasianum gives the full list, including the apocrypha "which are to be avoided by Catholics."
- Decretum Gelasianum: at The Latin Library.
- Decretum Gelasianum: in English.
- Review of Ernst von Dobschütz, Das Decretum Gelasianum de libris recipiendis et non recipiendis in kritischem Text Leipzig, 1912: F. C. Burkitt in Journal of Theological Studies 14 (1913) pp. 469–471.
Mwanzo * Kutoka * Walawi * Hesabu * Kumbukumbu * Yoshua * Waamuzi * Ruthu * Samueli I * Samueli II * Wafalme I * Wafalme II * Mambo ya Nyakati I * Mambo ya Nyakati II * Ezra * Nehemia * TobitiDK * YudithiDK * Esta * Wamakabayo IDK * Wamakabayo IIDK * Yobu * Zaburi * Methali * Mhubiri * Hekima DK * SiraDK * Wimbo Bora * Isaya * Yeremia * Maombolezo * BarukuDK * Ezekieli * Danieli * Hosea * Yoeli * Amosi * Obadia * Yona * Mika * Nahumu * Habakuki * Sefania * Hagai * Zekaria * Malaki
Alama ya DK inaonyesha vitabu vya deuterokanoni visivyopatikana katika matoleo yote ya Biblia.