Augustine Lyatonga Mrema

Kutoka Wikipedia, kamusi elezo huru
Jump to navigation Jump to search
Augustine Lyatonga Mrema
Mh. Mrema
Mh. Mrema
Mwenyekiti wa TLP
Tarehe ya kuzaliwa 1945
Mahali pa kuzaliwa Mkoa wa Kilimanjaro
Chama Chama cha Wafanyakazi Tanzania
Dini Mkristo
Elimu yake Chuo Kikuu cha Cambridge, Chuo Kikuu cha Pacific
Digrii anazoshika Sayansi ya Jamii
Kazi Mwanasiasa


Augustine Lyatonga Mrema (amezaliwa mwaka wa 1945) ni mwanasiasa nchini Tanzania na mwenyekiti wa chama cha TLP(Tanzania Labour Party - Chama cha Wafanyakazi Tanzania).

Maisha ya Mwanzo(Kw: ufupi)[hariri | hariri chanzo]

Augustine Mrema alizaliwa mwaka 1945, huko mkoa wa Kilimanjaro Tanzania, katika kijiji cha Kilaracha kilichopo katika Wilaya ya Moshi vijijini akiwa mzaliwa wa pili katika familia ya watoto watano ya Mzee Lyatonga Mrema.

Elimu[hariri | hariri chanzo]

Mwaka wa 1955 -1963 alianza masomo yake ya darasani mpaka shule ya kati katika Wilaya aliyopo huko huko mkoani Moshi vijijini. Ilivyofika mwaka wa 1964 mpaka 1965 Mrema alijiunga na Chuo cha Ualimu cha Mtakatifu Patrick. Tangu 1966 bwana mrema alikuwa mwanachama mkubwa wa CCM.

Baada ya kumaliza mafunzo yake ya Ualimu na kupata kazi Mrema alianza kuchukua mafunzo yake ya sekondari ambapo mwaka wa 1968 alifanya mtihani wake wa kidato cha nne, wakati huo mitihani ikitoka Chuo Kikuu cha Cambridge cha nchini Uingereza.

Mwaka wa 1970-71 alijiunga kwenye mafunzo maalumu ya siasa na uongozi katika Chuo cha Kivukoni na mwaka wa 1980 na 81 alienda nchini Bulgaria ambako alifanikiwa kutunukiwa Diploma ya sayansi ya Ustawi wa jamii na Utawala.

Kazi na Kujiendeleza Kielimu[hariri | hariri chanzo]

Augustine Lyatonga Mrema baada ya hapo alifanya kazi mbalimbali za kijamii na kichama kabla ya kujiunga na Chuo Kikuu cha Pacific mwaka 2003 ambako ametunukiwa Shahada ya Sanaa katika Sayansi ya Jamii.

Bwana Mrema alianza kazi mwaka 1966-69 kama mwalimu akifundisha shule mbalimbali za mkoa wa Kilimajaro, ilopofika mwaka 1972 na 1973 aliteuliwa kuwa mratibu wa elimu wa Kata.

Mwaka 1974 na 1980 Augustine Lyatonga Mrema alichaguliwa kuwa mwalimu wa siasa katika wilaya mbalimbali kwa niaba ya Chama cha Mapinduzi.

Mwaka wa 1980 na 1982 bwana Mrema alichaguliwa kuwa Mwalimu wa Chuo kikuu cha usalama wa Taifa na mwaka 1982 hadi 1984 bwana Mrema aliteuliwa kuwa Kaimu mkuu wa usalama wa Taifa kwa mkoa wa Dodoma, mwaka 1983 hadi 1984 aliteuliwa tena kuwa Katibu wa kikosi cha ulinzi na usalama makao makuu Dodoma.

Shughuli za Kisiasa[hariri | hariri chanzo]

Mwaka wa 1985 Mrema alirudi katika Jimbo lake na kugombea Ubunge huko alipata ushindi mkubwa tu, lakini hata hivyo aliwekewa pingamizi na Mahakama Kuu ya Kilimanjaro na wakati kesi ikiendelea Mrema alipelekwa katika mkoa wa Shinyanga, Wilaya ya Kahama kuwa Afisa Usalama wa Taifa katika wilaya hiyo, ilipofikia mwaka 1987 alishinda rufaa yake na kurejeshewa ubunge wake.

Aligombea ubunge kwa mara nyingine mwaka 1990 na akafanikiwa kutetea jimbo lake tena safari hiyo kwa kishindo na akarudi bungeni kwa mara ya pili.

Baadae akateuliwa kuwa Waziri wa Mambo ya Ndani kwa mwaka wa 1990 hadi 1994, na wakati huohuo mwaka 1993 hadi 1994 aliteuliwa tena kuwa Naibu Waziri Mkuu cheo ambacho hata hivyo hakikuwepo kwenye Katiba ya nchi.

Ilipofika mwaka 1994 alibadilishwa Wizara hiyo na kuhamishiwa katika Wizara ya Kazi, Maendeleo ya Vijana na Michezo.

Kujiengua na Chama Tawala[hariri | hariri chanzo]

Mh. Mrema alijiengua na CCM mwaka 1995 na kujiunga na Chama cha NCCR - Mageuzi ambako huko alienda kuwa Mwenyekiti wa Taifa na mgombea Urais kupitia chama hicho.

Mrema ambaye sasa ni Mwenyekiti wa Taifa wa Chama cha Tanzania Labour Part (TLP) aligombea urais mara mbili hiyo ilikuwa mwaka 2000 kupitia (TLP), na akagombea tena 2005 kwa mara ya tatu kupitia chama hicho cha TLP.