Nenda kwa yaliyomo

Athi

Kutoka Wikipedia, kamusi elezo huru
Muonekano wa Mto Athi

Athi ni jina la mto katika kaunti ya Kitui, Kenya, Afrika Mashariki. Sehemu za mto hujulikana pia kwa majina ya Galana na Sabaki, kwa hiyo mto wote huitwa pia Athi-Galana-Sabaki.

Ina urefu wa kilomita 390, na beseni lenye eneo la Km² 70,000.

Mto wa Athi umeupatia jina lake mji wa Athi River karibu na Nairobi pia kwa kampuni ya Athi River Mining.

Athi inaanza karibu na Nairobi ikielekea Bahari Hindi. Inapita Mbuga ya Kitaifa ya Tsavo Mashariki pia tambarare ya juu ya Yatta ilipotafuta njia yake kuvukia eneo kubwa la mawe ya kivolkeno.

Baada ya maporomoko ya maji ya Lugard inapokea mto Tsavo ikibadilika jina lake. Mto unaitwa kuanzia hapa kwa jina la Galana. Kabla ya kufika katika Bara Hindi karibu na Malindi upande wa kaskazini jina linabadilika tena kuwa Sabaki.

Tazama pia

[hariri | hariri chanzo]

Viungo vya nje

[hariri | hariri chanzo]