Mtume Andrea
Mitume wa Yesu |
---|
|
Mtume Andrea alikuwa Myahudi wa karne ya 1, mmoja kati ya wawili wa kwanza kati ya Mitume wa Yesu.
Anaheshimiwa na Wakristo wote kama mtakatifu, hasa tarehe 30 Novemba iliyo sikukuu yake[1].
Ni msimamizi wa Uskoti, Russia, Ugiriki, Romania, Malta, Prussia, wa jimbo la Konstantinopoli na wa mabaharia, wavuvi, na waimbaji.
Asili na jina
[hariri | hariri chanzo]Inakadiriwa alizaliwa mwaka 6 K.K. huko Bethsaida akauawa 60 hivi huko Patras (Ugiriki).
Jina lake asili la Kiyahudi halijulikani. Kwa Kigiriki aliitwa Ανδρέας (Andreas, maana yake Mwanamume, Rijali). Anaitwa pia Protocletos yaani Wa kwanza kuitwa (na Yesu Kristo).
Agano Jipya linasema Andrea alikuwa ndugu wa Mtume Petro, mwana wa Yona au Yohana (Math 16:17; Yoh 1:42).
Wito wake
[hariri | hariri chanzo]Wote wawili walihamia Kafarnaumu ili kufanya kazi ya uvuvi, na ndipo walipoitwa na Yesu kuwa "wavuvi wa watu" (ἁλιείς ἀνθρώπων, halieis anthropon).
Injili ya Yohane inaarifu kuwa Andrea aliwahi kuwa mwanafunzi wa Yohane Mbatizaji, mpaka nabii huyo alipomuelekeza amfuate Yesu Kristo, "Mwanakondoo wa Mungu" atakayekamilisha kazi yake mwenyewe (Yoh 1:35-40). Andrea akiwa wa kwanza kumtambua Yesu kuwa Masiya, alimtambulisha kwa ndugu yake hukohuko kwenye mto Yordani (Yoh 1:41).
Ni baada ya hapo kwamba waliitwa kuacha yote wamfuate Yesu (Mk 1:17-18; Math 4:19-20; Lk 5:11).
Baada ya ufufuko wa Yesu
[hariri | hariri chanzo]Katika Injili Andrea anatajwa mara kadhaa kuwa karibu sana na Yesu (Mk 13:3; Yoh 6:8, 12:22), lakini katika Matendo ya Mitume anatajwa mara moja tu, katika orodha ya Mitume (1:13).
Mwanahistoria Eusebius wa Kaisarea anataja Asia Ndogo, Skizia, pwani ya Bahari Nyeusi na mto Volga hadi Kiev kuwa mahali pa utume wake baada ya ufufuko wa Yesu.
Mapokeo mengine yanadai alifanya utume sehemu za Akaya (Ugiriki) akasulubiwa huko Patras juu ya msalaba wenye umbo la X uliopewa jina lake[2].
Apokrifa za Andrea
[hariri | hariri chanzo]Kati ya vitabu vilivyokataliwa na Kanisa (Decretum Gelasianum ya Papa Gelasio I) kuna Injili ya Andrea na Matendo ya Andrea vilivyoandikwa karne ya 3.
Picha
[hariri | hariri chanzo]-
Ndugu Limbourg, Kifodini cha Mt. Andrea, toka Les Très Riches Heures du duc de Berry, Chantilly, Musée Condé
-
José de Ribera, Kifodini cha Mt. Andrea, 1628, Budapest, Szépmüvészeti Múzeum.
-
Kifodini cha Mt. Andrea, karne XII, Presencio.
Tazama pia
[hariri | hariri chanzo]- Watakatifu wa Agano la Kale
- Orodha ya Watakatifu Wakristo
- Orodha ya Watakatifu wa Afrika
- Orodha ya Watakatifu Wafransisko
Tanbihi
[hariri | hariri chanzo]Marejeo
[hariri | hariri chanzo]Kwa Kiswahili
[hariri | hariri chanzo]- Thenashara, Mitume Kumi na Wawili – tafsiri ya P. A. Bunju – Toleo la pili – ed. Benedictine Publications Ndanda Peramiho – Ndanda 1984 – ISBN 9976-63-030-1
Kwa lugha nyingine
[hariri | hariri chanzo]- Metzger, Bruce M. (ed) (1993). The Oxford Companion to the Bible. Oxford, UK: Oxford University Press. ISBN 0-19-504645-5.
{{cite book}}
:|first=
has generic name (help); Unknown parameter|coauthors=
ignored (|author=
suggested) (help) - Attwater, Donald and Catherine Rachel John. The Penguin Dictionary of Saints. 3rd edition. New York: Penguin Books, 1993. ISBN 0-140-51312-4.
Viungo vya nje
[hariri | hariri chanzo]- The Missionary Journeys of the Apostle Andrew Archived 1 Desemba 2007 at the Wayback Machine.
- Texts of The Acts of Andrew The Acts and Martyrdom of Andrew and The Acts of Andrew and Matthew
- Saint Andrew in Orthodoxy Archived 2 Januari 2008 at the Wayback Machine.
- Andreas: The Legend of St. Andrew translated by Robert Kilburn Root, 1899, from Project Gutenberg
- Biographical Study on St. Andrew the Apostle Archived 28 Desemba 2007 at the Wayback Machine.
- Catholic Encyclopedia article
- The Life and Miracles of St. Andrew The Apostle Archived 2 Aprili 2010 at the Wayback Machine.
- St. Andrew in the National Archives of Scotland Archived 16 Septemba 2013 at the Wayback Machine.
- Paintings and Statues of Saint Andrew in Malta and around the world
- National Shrine to St Andrew in Edinburgh Scotland Archived 11 Agosti 2013 at the Wayback Machine.
- Scottish Government Celebrations of St. Andrew's Day
- Grimm's Saga No. 150 about St. Andrew Archived 21 Januari 2012 at the Wayback Machine.
- St. Andrew page Archived 23 Novemba 2011 at the Wayback Machine. at Christian Iconography
- "The Life of St. Andrew" Archived 23 Novemba 2011 at the Wayback Machine. from Caxton's translation of the Golden Legend
Makala hii kuhusu mtu wa Biblia bado ni mbegu. Je, unajua kitu kuhusu Mtume Andrea kama habari za maisha au kazi yake? Labda unaona habari katika Wikipedia ya Kiingereza au lugha nyingine zinazofaa kutafsiriwa? Basi unaweza kuisaidia Wikipedia kwa kuihariri na kuongeza habari. |