Wikipedia:Jumuiya/Kumbukumbu Julai 2008 hadi Desemba 2009

Kutoka Wikipedia, kamusi elezo huru

Hii ni kumbukumbu ya ukurasa wa jumuiya Julai 2008 hadi Septemba 2009

"Jumuiya" ya awali angalia hapa: Wikipedia:Jumuia/Kumbukumbu_hadi_JUlai_2008

Rudi kwenye Wikipedia:Jumuiya


Manual for new and small Wikipedias[hariri chanzo]

Hello, at Meta there are pages created to help new and small Wikipedias: Manual and Wikipedia and help pages. You are welcome to have a look and comment. Kind regards --Ziko (majadiliano) 22:56, 15 Agosti 2008 (UTC)[jibu]


Suricata[hariri chanzo]

Sorry for not speaking your beautiful language. Can anybody just start a page about the en:meerkat or es:suricata? It is there stated that the word comes from Kiswahili and, (for wikipedias in all the languages that borrow this word from Kiswahili, even Latin), it's very confusing not having a Kiswahili article for that. Starting even only with the name can clarify a lot. And I think it a Kiswahili word so widespread all over the world that is emblematic enough to (must) be in your wiki. Many thanks from all languages. en:Sobreira

Actually, it comes from the Dutch word "Meer Kat" (lake cat). A native Dutchie called Sjorskingma (majadiliano) 12:16, 14 Novemba 2009 (UTC)[jibu]
I'm pretty sure he meant that the word "suricata" was borrowed from Swahili, not "meer kat". Jon Harald Søby (majadiliano) 02:25, 16 Novemba 2009 (UTC)[jibu]
Hakika si vile. Linganisha "Meerkat" kwenye en-wikipedia: ""Meerkat" is a loanword from Afrikaans. The name has a Dutch origin but by misidentification. Dutch meerkat refers to the "guenon", a monkey of the Cercopithecus genus. The word "meerkat" is Dutch for "lake cat", but the suricata is not in the cat family, and neither suricatas nor guenons are attracted to lakes; the word possibly started as a Dutch adaptation of a derivative of Sanskrit markaţa मर्कट = "monkey", perhaps in Africa via an Indian sailor on board a Dutch East India Company ship. The traders of the Dutch East India Company were likely familiar with monkeys, but the Dutch settlers attached the name to the wrong animal at the Cape. The suricata is called stokstaartje = "little stick-tail" in Dutch." halafu pia http://en.wiktionary.org/wiki/Suricata: "Latin "Syria" and "cat"; Sometimes an etymology from a Swahili "rock-cat" has been claimed which, however, is erroneous. The Latin etymology leaves the question open, why an animal that only lives in Southern Africa has been called "Syrian cat"." --Kipala (majadiliano) 15:16, 16 Novemba 2009 (UTC)[jibu]

Takwimu[hariri chanzo]

Orodha ya Wikipedia:Makala za msingi za kamusi elezo ambayo ni sawa na meta:List of articles every Wikipedia should have ni msingi wa jedwali inayolinganisha ubora wa wikipedia katika lugha mbalimbali. Napenda kuonyesha maendeleo ya wikipedia yetu kwa kutunza kumbukumbu ya jedwali ile kwa sw-wikipedia na matokeo yake ya kila mwezi. Jedwali yote inaonekana kwa orodha hii --Kipala (majadiliano) 11:26, 31 Desemba 2008 (UTC)[jibu]

Mwezi Nafasi Wiki Language Weight Average Article Size Absent (0k) Stubs
(< 10k)
Articles
(10-30k)
Long Art.
(> 30k)
Score Growth
29 Novemba 2008 65 sw Kiswahili 1.0 3,173 392 594 13 1 7.28 +0.35
3 Januari 2009 60 sw Kiswahili 1.0 3,181 300 681 17 2 8.52 +1.24


2 Februari 2009 60 sw Kiswahili 1.0 3,196 284 697 17 2 8.70 +0.18
2-3 Mei 2009 61 sw Kiswahili 1.0 3,128 301 680 17 2 8.51 -0.18

Ukurasa wa BOT[hariri chanzo]

Salam nyingi Wanawikipedia! Nimejaribu kuangalia mawili matatu kuhusu ukurasa wa Mabot naona hapa hamna kabisa. Kikawaida BOT huwa na ukurasa maalum wa kuombea na sio katika ukurasa mkuu wa JUMUIA. Ningeshauri hizi BOT ziwekewe ukurasa wao - kwa mafano: Wikipedia:Bot kama wanavyofanya kule katika Meta na Wikipedia kwa Kiingereza! Sijui mnaonaje wandugu?--41.204.128.101 08:37, 4 Januari 2009 (UTC)[jibu]

Naunga mkono hoja hii --Mwanaharakati (Longa) 10:21, 5 Januari 2009 (UTC)[jibu]
Namshukuru Kipala kwa kuanzisha ukurasa huu. Asante sana!!! --Baba Tabita (majadiliano) 08:21, 23 Januari 2009 (UTC)[jibu]

Betawiki update[hariri chanzo]

Sera ya faragha[hariri chanzo]

Nimefuta maandishi yaliyokuwepo kwenye ukarasa wa sera ya faragha na kuweka kiungo kwenye ukurasa wa sera kule Wikimedia Foundation, hadi itakapopatikana kwenye Kiswahili. Lloffiwr (majadiliano) 19:54, 22 Februari 2009 (UTC)[jibu]

Kutafsiri jumbe[hariri chanzo]

Nimeanza kuweka mapendekezo ya kutafsiri jumbe za Wikipedia (jumbe ni yale maneno yanayoonekana kwenye kusano wa Wikipedia, kwa mfano, 'ukurasa wa mradi', 'majadiliano', nk yalioandikwa juu ya ukurasa huu) kwenye kona ya majadiliano. Sipendi kuanza kubadilisha jumbe zilizopo tayari bila kutoa nafasi, jumuia ijadili mapendekezo haya, hasa kwa sababu mimi si Mswahili, nimejifunza Kiswahili tu. Nimeamua kuandika haya maneno ili kutangaza kwamba nafasi ya kujadiliana mambo haya ipo kwenye Kona ya Majadiliano. Nitafurahi kusoma mawazo ya wengine wenu. Lloffiwr (majadiliano) 19:10, 30 Machi 2009 (UTC)[jibu]

Jamii:Mbegu[hariri chanzo]

Hi, we need many more categories for stubs. Now, we have Jamii:Mbegu + 2 Tanzanian categories. We need especially stub categories for people and for jiografia. Thank you. --Mr Accountable (majadiliano) 10:39, 15 Juni 2009 (UTC)[jibu]

Okay, I started people stubs with Chinua Achebe as example, and geography stubs with Aachen as example. Simply use {{mbegu-mtu}} and {{mbegu-jio}}. All the best! --Baba Tabita (majadiliano) 16:09, 15 Juni 2009 (UTC)[jibu]
Could there be a few more at this time? There seem to be 1000s of stubs. Maybe Jio: {{mbegu-Afrika-jio}}, {{mbegu-Ulaya-jio}} and {{mbegu-Asia-jio}}? And {{mbegu-mmea}}, {{mbegu-mnyama}} {{mbegu-sayansi}} {{mbegu-michezo}} and {{mbegu-serikali}}? Meanwhile, I'll start up with sorting the stubs. --Mr Accountable (majadiliano) 16:35, 15 Juni 2009 (UTC)[jibu]
And, after doing this for an hour, maybe 3 more: {{mbegu-Tanzania-jio}}/{{mbegu-jio-Tanzania}}, "scientist" and "Roman Catholicism". Thanks. --Mr Accountable (majadiliano) 18:51, 15 Juni 2009 (UTC)[jibu]
Tanzanian geography stubs already exist. They used to be called {{tanzania-geo-stub}}. I've just renamed that to {{mbegu-jio-TZ}}. I'll let you know once I've created some others, presumably {{mbegu-jio-Afrika}}, {{mbegu-jio-Ulaya}} and {{mbegu-jio-Asia}}, as requested. Thanks again! --Baba Tabita (majadiliano) 19:05, 15 Juni 2009 (UTC)[jibu]
That's very great. And, since there's 3,000 to go, suggestions include: {{mutribu}}, {{mwandishi}}, {{mbegu-jio-Marekani}}, {{mbegu-mto}},{{mbegu-sinema-kuigiza...}} Thanks again. --Mr Accountable (majadiliano) 19:11, 15 Juni 2009 (UTC)[jibu]
Or maybe national stubs, as {{mbegu-Nigeria}}, {{mbegu-Kenya}} {{mbegu-Ujeramani}}, {{mbegu-Uturuki}}.....etc. --Mr Accountable (majadiliano) 19:17, 15 Juni 2009 (UTC)[jibu]
Whoa! I've done the continents: see Aachen for Europe, Bangkok for Asia, and Kairo for Africa. I'll let you know about national geography stubs and subcategorised people stubs in due course. --Baba Tabita (majadiliano) 19:26, 15 Juni 2009 (UTC)[jibu]
Maybe I've made too many suggestions; let me make a short-list of just 3 at this particular time: "Scientist", "Musician" and "Writer". There are very many more mbegu-mtu than there are mbegu-jio, and there are very many mbegu-jio. Cheers. --Mr Accountable (majadiliano) 19:29, 15 Juni 2009 (UTC)[jibu]
No prob :-) In the meantime, I've done {{mbegu-jio-KE}} for Kenya (cf Malindi), {{mbegu-jio-Nigeria}} (cf Lagos) and {{mbegu-jio-USA}} (cf New Jersey). I'll turn to people now. Cheers, too! (If only I *did* have a cool lager here ...) --Baba Tabita (majadiliano) 19:45, 15 Juni 2009 (UTC)[jibu]
Your three requests are done: {{mbegu-mwanasayansi}} for scientists (cf Hans Buchner), {{mbegu-mwandishi}} for writers (cf Orhan Pamuk) and {{mbegu-muziki}} for musicians (cf Ludwig van Beethoven). That'll have to do for tonight. Good night! --Baba Tabita (majadiliano) 20:08, 15 Juni 2009 (UTC)[jibu]
For reference purpose's sake, here are two more people stub templates I did: {{mbegu-Nobel}} for scientists who won the Nobel Prize (cf Hans Georg Dehmelt), and {{mbegu-mwanasiasa}} for politicians (cf Harry S. Truman). Cheers. --Baba Tabita (majadiliano) 06:22, 16 Juni 2009 (UTC)[jibu]
And the next batch: {{mbegu-mmea}} for plants (cf Muhogo), {{mbegu-igiza-filamu}} for film actors (cf Anne Mwampamba), {{mbegu-dini}} for general religion stubs (cf Ujain), {{mbegu-Papa}} for Popes (cf Papa Honorius III), and in between {{mbegu-Ukristo}} for Christianity in general, {{mbegu-Mkristo}} for Christian biography stubs, and {{mbegu-katoliki}} for the Roman Catholic Church in general. That should keep you busy for a while ;-) Thanks for the great job you're doing! --Baba Tabita (majadiliano) 07:55, 16 Juni 2009 (UTC)[jibu]
Yes, I'm sorting stubs. All I can ask now is for {{mbegu-jio-China}} and {{mbegu-jio-Japani}}. I don't suppose it would be a problem if I started using these labels before the stub files is created, would it? --Mr Accountable (majadiliano) 17:04, 16 Juni 2009 (UTC)[jibu]
I've received some complaints about kaizeri labeled as mbegu-mwanasiasa; I think we need a mbegu Kaizer and mbegu Roman Emperor label now. And maybe {{mbegu-Amerika, China, Japani, Mexiko and Uturuki}}. --Mr Accountable (majadiliano) 20:07, 16 Juni 2009 (UTC)[jibu]
Other possibilities include: {{mbegu-jio-karibi}}, {{mbegu-jio-Amerika-kati}}, {{mbegu-jio-Amerika-kusini}}, {{mbegu-jio-Kanada}}. I'm not sure which ones are more important. If one goes ahead with Ujeramani ya Majimbo or Ufaransa ya Majimbo, those would need stub categories as well. --Mr Accountable (majadiliano) 21:50, 16 Juni 2009 (UTC)[jibu]
Ready for use are: {{mbegu-jio-China}}, {{mbegu-jio-Japani}}, {{mbegu-jio-Uturuki}}, {{mbegu-jio-Ujerumani}}, {{mbegu-jio-Ufaransa}}, {{mbegu-jio-Kanada}}, and {{mbegu-jio-Mexiko}}. Cheers! --Baba Tabita (majadiliano) 13:29, 17 Juni 2009 (UTC)[jibu]
Kaizer/Emperor stubs, I subcategorised immediately - for Ancient Rome, use {{mbegu-Kaizari-Roma}}, for Byzantium {{mbegu-Kaizari-Byzant}}, for Japan {{mbegu-Kaizari-Japani}}, for Ethiopia {{mbegu-Kaizari-Uhabeshi}}, and for Germany {{mbegu-Kaizari-Ujerumani}}. Happy stub-sorting! --Baba Tabita (majadiliano) 14:00, 17 Juni 2009 (UTC)[jibu]

And more stub templates: education {{mbegu-elimu}}, culture {{mbegu-utamaduni}} plus Tanzanian culture separately {{mbegu-utamaduni-TZ}}, science {{mbegu-sayansi}}, biology {{mbegu-biol}} plus animals {{mbegu-mnyama}}, chemistry {{mbegu-kemia}}, and physics {{mbegu-fizikia}}. Enjoy! --Baba Tabita (majadiliano) 07:22, 18 Juni 2009 (UTC)[jibu]

Oh, and not to forget: Politics {{mbegu-siasa}}. --Baba Tabita (majadiliano) 08:18, 18 Juni 2009 (UTC)[jibu]

The next batch: for Bible stubs {{mbegu-Biblia}}, separated into Old {{mbegu-AganoK}} and New Testament {{mbegu-AganoJ}}, plus Bible characters {{mbegu-mtu-Biblia}} (a category strangely absent from en:wp). I've also subcategorised writers: from the US {{mbegu-mwandishi-USA}}, from Europe {{mbegu-mwandishi-Ulaya}}, from Africa {{mbegu-mwandishi-Afrika}}; musicians from the US {{mbegu-muziki-Marekani}}, from Europe {{mbegu-muziki-Ulaya}}, from Africa {{mbegu-muziki-Afrika}}; scientists from the US {{mbegu-mwanasayansi-USA}}, and film actors from the US {{mbegu-igiza-filamu-USA}}. All for now. --Baba Tabita (majadiliano) 08:57, 19 Juni 2009 (UTC)[jibu]

Makala ya Wiki/Mwanzo[hariri chanzo]

Salam nyingi Wanawikipedia! Hizi ni taarifa kuhusu kubadilisha makala ya wiki ya Wikipedia. Kwa yeyote atakayehitajia kubadilisha makala ya wiki, basi anatakiwa aje hapa. Ukibadilisha hapo - kule yenyewe itaonyesha kurasa mpya na si kama zamani tena!!! Basi nimeweka maelezo haya hapa ili iwe faida kwa wale wote wenyekutaka kubadilisha ukurasa ule. Pia, endapo maombi yatakuwa meengi, basi tunaweza kuanzisha kitu kama "queve" au "foleni" ya makala zitakazokaa usoni kule. Foleni kwa makala maalum, labda tuiumbe hapa - kama jinsi wenzetu wanavyofanya! Ahsanteni sana. Wenu kijana mtiifu,Muddybau,--Mwanaharakati (Longa) 13:05, 22 Juni 2009 (UTC)[jibu]

Racibórz[hariri chanzo]

Hi. Can somebody write an (at least ;] ) short stub about my city (Racibórz) on your Wikipedia? Many thanks for anyone who could do that :) Olos88 (majadiliano) 07:44, 27 Julai 2009 (UTC)[jibu]

Small request[hariri chanzo]

Hello! I am a Polish wikipedian and I would like to ask you for writing a new article about former Polish President who won the Nobel Peace Prize in 1983 – Lech Wałęsa. I have looked for his article in your Wikipedia but without success. Polish Wikipedians will be grateful for your help. Thank you so much in advance! PS article in English you can find here. Best wishes from Poland, Patrol110 (majadiliano) 21:07, 21 Septemba 2009 (UTC)[jibu]

The LocalisationUpdate extension has gone live[hariri chanzo]

The LocalisationUpdate extension is now enabled for all Wikimedia projects. From now on new localisations that become available in SVN will become available to your project within 24 hours. Your localisations get into SVN from translatewiki.net typically within a day and at worst in two days. This is a huge improvement from the old practice where the localisations became available with new software. This could take weeks, even months.

The localisations done by our community at translatewiki.net are committed to SVN typically every day. When the system messages in English are the same as the local messages, they will now be inserted in a file and are available for use in all our projects in a timely manner

What this means for you[hariri chanzo]

Local messages have an impact on the performance of our system. It is best when messages are as much as possible part of the system messages. In order to remove unnecessary duplication, all the messages that have a local localisation and are exactly the same as the system message will be removed. What we ask you to do is to compare and proof read the messages in translatewiki.net and the local messages. You can then either remove local messages when the translatewiki.net message is to be preferred or, you can update the message at translatewiki.net.

Messages that are specific to your project will have to stay as they are. You do want to check if the format and the variables of the message are still the same.

Why localise at translatewiki.net[hariri chanzo]

When you localise at translatewiki.net, your messages will be used in all Wikimedia projects and eventually in all MediaWiki based projects. This is how we provide the standard support for your language. When messages change, at translatewiki.net you will be prompted to revisit your translations. Localising is more efficient because we have innovated the process to make you more efficient; there is text explaining about messages and we have applied AJAX technology to reduce the number of clicks you have to make.

Translatewiki.net update[hariri chanzo]

How can we improve the usability for your language[hariri chanzo]

We expect that with the implementation of LocalisationUpdate the usability of MediaWiki for your language will improve. We are now ready to look at other aspects of usability for your language as well. There are two questions we would like you to answer: Are there issues with the new functionality of the Usability Initiative Does MediaWiki support your language properly

The best way to answer the first question is to visit the translatewiki.net. Change the language to your language, select the “vector” skin and add the advanced tool bar in in the preferences and check out the new functionality. And make some changes in your user page. When there is a need to improve on the localisation, please make the necessary changess . It should update your localisation straight away. We would like you to report each issue individually at http://meta.wikimedia.org/wiki/Usability_issues.

When there are problems with the support of MediaWiki for your language, we really want to know about this. It is best to report each issue separately. In this way there will be no large mass of issues to resolve but we can address each issue on its own. Consider issues with the display of characters, the presentation of your script, the position of the side bar, the combination of text with other languages, scripts. It is best to try this in an environment like the prototype wiki as it provides you with a clean, basic and up to date environment. The prototype wiki is available for five languages but you can select any of them, change the preferences to your language and test out MediaWiki for your language.

We would like you to report each issue individually at http://meta.wikimedia.org/wiki/Language_issues. The issues you raise will all be assessed. It is important to keep each issue separate, because this will make it easier to understand the issues and find solutions.

PS This text has been approved by Naoko, Brion and Siebrand. Thanks, GerardM (majadiliano) 18:45, 30 Septemba 2009 (UTC)[jibu]


Istilahi ya wikipedia[hariri chanzo]

Wapendwa wakabidhi na watumiaji wenzangu,

Tangu awali nimesikitika na utafsiri wa istilahi fulani ya wikipedia yetu. Mara kwa mara, utafsiri huo umetegemea bidii ya mtu mmoja au wawili tu bila uchunguzi wa ndani, tena bila utaalamu wa elimu tafsiri. Kwa hiyo naona umuhimu wa kutafiti istilahi yetu, na kubadilisha sehemu zisizofaa.

Kwa leo nashika fursa hii kuwapelekea changamoto: Kwa kweli, tukilinganisha maana ya "Category" katika lugha ya Kiingereza, na maana ya "Jamii" katika lugha ya Kiswahili, naona kama hatujapata utafsiri fasaha. K.m. tukiangalia tendo la "categorize", bila shaka tunapata "kuainisha" kwa Kiswahili (au labda kupambanua au kubainisha). Sasa, pendekezo langu hasa ni kutumia "Aina" kwa ajili ya "Category", hasa kwa vile "Category" inaonyesha aina ya makala.

Ingekuwa hata vizuri zaidi tukiweza kujenga msingi imara wa maamuzi yetu ya istilahi humo. Je, utafiti wa matumizi ya lugha ya Kiswahili unapatikana, labda kutoka kwa mashirika kama kamusi.org ya mwenzetu Bw.Malangali? Kabla hatujabadilisha istilahi yoyote, bora tutafute na kuchunguza matokeo ya utafiti kama upo.

Ni wenu katika uboreshaji wa wikipedia yetu, --Baba Tabita (majadiliano) 09:32, 23 Oktoba 2009 (UTC)[jibu]

Haya, unaona kutumia neneo "aina" ni afadhali zaidi kuliko labda "kundi?" Katika kutaja aina hizi za makala, sidhani kwamba "aina" ni nzuri kuwa badala ya "jamii". Mafano: "kundi:Wanamuziki wa Tanzania" ni bora zaidi ya "aina:Wanamuziki wa Tanzania". Yaani, tuandike "kundi" badala ya aina. Sijui, lakini ukienda sana kiundani utaona HATA "jamii" nayo iko sawa tu. Ila, ikionekana kwamba haipo kwenye mfumo unaotakiwa, basi ibadilishwe.--Muddyb MwanaharakatiLonga 11:58, 23 Oktoba 2009 (UTC)[jibu]
Nilivyoambiwa na Bwana Muddyb sasa hivi, mwaka wa 2006 kulikuwa na mjadala mfupi kuhusu mada hiyo. Naomba muurejelee. Asante! --Baba Tabita (majadiliano) 13:42, 23 Oktoba 2009 (UTC)[jibu]

::::Majadiliano ya mwaka 2006 kuhusu jamii, kundi, category

Nimeona sasa tu ya kwmaba "category" imetafsiriwa kwa "babu". Sidhani ya kwamba inafaa. Haieleweki. "Jamii" au "Kundi" ni sawa. Kamusi zote za TUKI hazina Babu kwa maana hiyo, iko katika Madan-Johnson tu. --Kipala 18:31, 19 Aprili 2006 (UTC)
Ni poa tu. Mimi nilitumia "Kamusi Project" kwa kutafsiri "Category", lakini ukiamini kwamba haifai, unaweza kuibadilisha iwe "Jamii" au "Kundi". Mimi ningependelea "Jamii", lakini sina uhakika. Marcos 14:03, 20 Aprili 2006 (UTC)
Nitaje "aina" na "jinsi" pia, lakini sijui kamwe zikifaa. Matt Crypto 23:34, 20 Aprili 2006 (UTC)

Nimeingiza majadiliano ya kale hapo.

  • Kwanza tunaona ya kwamba "jamii" si ufunuo kutoka mbinguni lakini ilikuwa chaguo katika majadiliano ya wanaWikipedia watatu.
  • Pili azimio halikuwa la uhakika.
  • Tatu moyo wangu sipendezwi na "aina" ila tu sina uhakika. Nadhani katika sentensi ni sawa kabisa kusema "Ng'ombe huhesabiwa katika aina ya wanyama wanaoitwa mamalia". Ila tu kwa kifupi kusema "Ng'ombe yuko katika aina ya mamalia" ???? "Yuko katika kundi..." sawa.
  • Nne naomba tueleze vizuri zaidi ni nini kinachokusumbua kuhusu neno "Jamii" ? Nikisoma "kamusiproject" vema ni pia chaguo la mradi wa kilinux. Yaani unataja sababu mmoja ya "categorize" imechukuliwa kama "kuainisha". Sawa lakini tatizo ni nini?

Hebu tuendelee kushauriana. --Kipala (majadiliano) 21:44, 23 Oktoba 2009 (UTC)[jibu]


Kwanza nawashukuru na kuwapongeza waanzilishi wa Wikipedia ya Kiswahili na wale wote waliochangia juhudi zao.

Pamoja na hayo, bado kuna makosa ya wazi, kwa mfano: ukarasa, masahihisho zangu, n.k. Pia watumiaji wasiojua lugha yetu hata kidogo wanatunga kurasa bomu. Hatupendi kuwakatisha tamaa, lakini kusahihisha michango yao ni vigumu, kwa sababu pengine hatuelewi walitaka kuandika nini au hata kichwa chenyewe. Kuhusu istilahi, ni kweli tunahitaji kwenda pamoja. Nionavyo mimi, jamii inafaa kuliko aina. Kuainisha ni kugawa jamii, kumbe jamii ni kundi la aina. Kwa mfano, Maharagwe ni aina ya nafaka za jamii ya kunde. Jamii ya kunde ina aina mbalimbali: kunde, maharagwe, choroko n.k. --Riccardo Riccioni (majadiliano) 04:32, 25 Oktoba 2009 (UTC)[jibu]

Kwa kweli mimi sioni tatizo kwa "jamii" na sipendi sana "aina". Tukiainisha vitu tunaviweka kwa makundi au jamii. Kila jamii ina ndani yake vitu vya aina moja. Napendekeza tuendelee na "jamii", lakini mukiipenda sana tutumie "kundi". ChriKo (majadiliano) 15:17, 25 Oktoba 2009 (UTC)[jibu]
Baada ya kusoma majadiliano ya juu nisingeona vibaya jina libadilishwe kuwe kundi, au hata aina (labda). Lakini 'jamii' nalo si mbaya. Kwa hiyo, labda ingekuwa vyema isibadilishwe - ibaki jamii tu!
Niongeze hapa kwamba 'jamii' ni moja ya maeneo ya wiki. Siku hizi majina ya maeneo ya wiki hutafsiriwa kule translatewiki.net (kwa ajili ya watumiaji wasioijua hiyo tayari). Sasa hivi tupo wanne tuliojiunga na translatewiki.net ili tutafsiri katika Kiswahili. Maombi ya kutafsiri majina ya wiki au mambo mengine yanayohusu kusano ya miradi yote ya Mediawiki yanaweza kupelekwa kule au yanaweza kujadiliwa hapa kwa kirefu. Kazi ya kutafsiri jumbe inaenda taratibu tu shauri ya kuwa na watumiaji wachache walio na wajibu wengi au walio na nafasi ndogo tu ya kuchangia. Ni kweli kabisa kwamba kuna kazi kubwa ya kurekebisha jumbe pamoja na kuzitafsiri zile ambazo hazijatafsiriwa bado, kama ilivyotajwa juu!
Shida hasa ya kutafsiri category ni kwamba hakuna tayari neno la Kiswahili ambalo maana yake ni 'category' tu - yaani 'jamii', 'kundi' na 'aina' yote ni maneno yenye maana tofauti ya kimsingi, tunayoyaazima au kutohoa kuwa istilahi ya wiki. Ni vigumu sana kupata neno moja ambalo wote tutaridhika nalo, nadhani! Kwa hiyo kuyajadili istilahi yetu kati ya watumiaji wengi iwezekanavyo ni vizuri, hasa wakati wa kutunga neno jipya kabisa ambalo bado halipatikani kwenye kamusi yoyote.
Kutokana na shida hii ya kuchagua na kutunga istilahi mbalimbali, naona kwamba ingetusaidia sana kuwa na 'orodha ya istilahi' kwa ajili ya kueleza maana ya istilahi yetu. Nimeweka mada mpya ili kuijadili pendekezo hilo. Lloffiwr (majadiliano) 16:49, 25 Oktoba 2009 (UTC)[jibu]

Wapendwa, nimepeleka swali huko Jamiiforums, uwanja wa lugha. Tafadhali mwangalie hapa. Mchangiaji wa mwisho (Bw mwanakijiji) ambaye namwona anajua lugha kushinda wengi anashauri "Nadhani ukitumia "Fungu" unaweza kuwa karibu zaidi lakini vile vile kutumia "kundi' japo kwenye kiingereza bado una maneno mengi zaidi." --Kipala (majadiliano) 20:54, 25 Oktoba 2009 (UTC)[jibu]

Pia labda mwone Uainishaji wa kisayansi. Maana wengi walitumia mifano ya kuainisha. Kama maelezo haya yanafaa naona "KUNDI" linaweza kufaa zaidi (ingawa sioni shida ubwa kuhusu jamii).--Kipala (majadiliano) 04:22, 26 Oktoba 2009 (UTC)[jibu]
Duh! Haya, naona yule aliyechagua "fungu" hakujua namna ya mazingira ya neno lenyewe lilipo! Kumbe, ukiangalia na kufikiria utaona wote wanarudia kwenye "jamii" au "kundi". Labda niseme tu, hii si kazi ndogo kama jinsi tunavyofikiria kwa sasa. Madhara yake ni makubwa nifikiria kazi ya kutoa neno "jamii" kule kwenye translatewiki.net. Pia, hata hapa kwetu. Makala nyingi zilishaandikwa "jamii:fulani na fulani - yaani sijui ni kiasia gani lakini zaidi ya 2,000. Kumbuka kwamba, ukibadili mfumo wa category na kuuweka mwingine, basi zile makala zoote zitakuwa hazina jamii tena na idadi ya lundiko la makala kwenye kila jamii litapungua. Pia, kutakuwa na mchanganyo mwingi katika kila makala zilizoandikwa "jamii". Tafakarini, mkiona inafaa kubadili hata kama makala zitapotea, basi twendeni.--Muddyb MwanaharakatiLonga 06:16, 26 Oktoba 2009 (UTC)[jibu]
Nimefurahi sana kuona mjadala wa ndani kabisa. Hongereni na asanteni! Baada ya kusoma yote, hata mimi sioni shida kuendelea na neno la "jamii". Ila sasa, uamuzi huo umeimarishwa na jamii ya wanawikipedia wote (angalao wote ambao huchapa kazi humo mara kwa mara). Tuendelee na istilahi nyingine (kwa kuangalia michango ya hapo chini). Wasalaam, --Baba Tabita (majadiliano) 09:12, 26 Oktoba 2009 (UTC)[jibu]

Orodha ya istilahi za wiki[hariri chanzo]

Napendekeza tuwe na orodha ya istilahi za wiki ambaye itorodhesha istilahi zinazotumika kwenye wiki hii pamoja na kutoa maelezo ya maana zao. Tayari ipo orodha kadhalika kule Wikipedia ya Kiingereza. Ninapendekeza kwamba tuaanzishe ukurasa mpya unaoitwa 'Istilahi za wiki'. Tungeweza kuweka nakala ya 'Glossary' ya Kiingereza kuwa ukurasa mtoto ('subpage' - mnaonaje kutumia 'ukurasa mtoto' kwa ajili ya 'subpage'?) wa ukurasa wa 'istilahi za wiki'. Ukurasa uwekwe kwenye jamii ya 'msaada'. Pia mnaonaje tuweke kiungo upande wa kushoto kwenye sanduku la 'safari' ili ukurasa upatikane kila wakati kirahisi? Nipo tayari kuuanzisha ukurasa huu, ukikubalika, ila nafasi ya kuandika ukurasa nadhani sitakuwa nayo. Lloffiwr (majadiliano) 16:49, 25 Oktoba 2009 (UTC)[jibu]

Asante kwa wazo zuri kabisa! Naomba uuanzishe ukurasa ulivyoeleza, nasi wakabidhi wenzako tutajitahidi kuongezea orodha. Ninavyoeleza hapo chini, jamii ya {{jaribio}} haitatosha. Katika orodha, labda tuwe na safu inayotaja kiungo kwenda ukurasa husika kama mfano unaoonyesha istilahi yenye mashaka. Asante! --Baba Tabita (majadiliano) 10:12, 26 Oktoba 2009 (UTC)[jibu]
Mtumiaji:Lloffiwr, unadhani inafaa kutulisha keki halafu ikifika karibu na mdomo unairudisha? Rejea maelezo yako: Nipo tayari kuuanzisha ukurasa huu, ukikubalika, ila nafasi ya kuandika ukurasa nadhani sitakuwa nayo. Hii si vyema. Itakuwa vizuri zaidi uanzishe halafu siye wengine tutamalizia! Hapo je?--Muddyb MwanaharakatiLonga 10:25, 26 Oktoba 2009 (UTC)[jibu]
Ukurasa umeanzishwa. Kazi njema kwa wale watakaoandika maelezo ya istilahi. Bwana Mwanaharakati - nitashukuru ukiwa na nafasi ya kuhakikisha kwamba hakuna makosa ya sarufi humo. Mtaona kwamba nimeandika faharasa (TOC) mpya yenye herufi zinazotumika kwenye kiswahili tu. Ni sawa? Lloffiwr (majadiliano) 13:16, 1 Novemba 2009 (UTC)[jibu]
Haya, nimetazama uanzilisho ule - na nimeanza kutazama istilahi kama jinsi ulivyoeleza! Ahsante kwa kazi yako!!!--Muddyb MwanaharakatiLonga 05:58, 2 Novemba 2009 (UTC)[jibu]

Majina ya maeneo ya wiki[hariri chanzo]

Napendekeza kwamba tubadilishe majina ya maeneo ya wiki ya majadiliano kama ifuatavyo:

  • Majadiliano faili → Majadiliano ya faili
  • Wikipedia majadiliano → Majadiliano ya Wikipedia
  • MediaWiki majadiliano → Majadiliano ya MediaWiki
  • Kigezo majadiliano → Majadiliano ya kigezo
  • Msaada majadiliano → Majadiliano ya msaada
  • Jamii majadiliano → Majadiliano ya jamii

Lloffiwr (majadiliano) 17:37, 25 Oktoba 2009 (UTC)[jibu]

Kumbe, hizi zilitafsiriwa kwa pupa! Ukitazama kwa undani utaona hilo ulilosema ni sahihi. Hivyo, badilisha tu kwa mahali pa-pya.--Muddyb MwanaharakatiLonga 06:18, 26 Oktoba 2009 (UTC)[jibu]
Safi kabisa!!! Bahati mbaya sijagundua njia ya kubadilisha majina ya maeneno :( Kazi njema! --Baba Tabita (majadiliano) 10:53, 26 Oktoba 2009 (UTC)[jibu]
Bahati nzuri najua namna ya kubadilisha 'magic words' kama majina ya maeneo kule translatewiki.net! - kwa hiyo nitatekeleza. Lloffiwr (majadiliano) 14:21, 26 Oktoba 2009 (UTC)[jibu]
Majina mapya ya maeneo ya wiki yameshawekewa kule translatewiki.net lakini inaweza kuchukua wiki kadhaa kabla hazijaonekana hapa kwenye Wikipedia ya Kiswahili. Kama nimeelewa sana hapatakuwa na haja ya kurekebisha viungo vyovyote hapa - kompyuta itaelewa majina ya zamani pamoja na majina mapya. Lloffiwr (majadiliano) 17:42, 1 Novemba 2009 (UTC)[jibu]
Enhee, kumbe, zile taarifa za kubadilishwa kwa jumbe za Mediawiki kwenye maiwikipedia hapa kwetu hazijafika. Lakini nilipata taarifa hizo na Bwan Gerard Meijssen - tuliongea kupitia skype. Yaani, kifupi sasa hivi jumbe ikibadilishwa leo, basi baada ya siku mbili hadi tatu zinakuwa tayari zishabadilika hadi hapa kwetu - hivyo hatuna wasiwasi juu ya hilo!.--Muddyb MwanaharakatiLonga 06:04, 2 Novemba 2009 (UTC)[jibu]

Kutunga maneno mapya kwenye makala[hariri chanzo]

Kuhusu maneno mapya - nimetaja shida tulionayo ya kutunga istilahi za Wikipedia kwenye mada ya juu. Shida ya kutunga ipo pia katika makala. Kule kwenye Wikipedia ya Kiwelisi tumeanzisha taratibu ya kutunga maneno ili watumiaji waweze kutunga, halafu wengine wapate nafasi ya kujadili maneno haya, na kuyabadilisha. Taratibu ni hivyo:

Wakati wa kutunga maneno mapya tunaingiza kigezo mwishoni mwa makala ambacho kinajulisha kwamba kuna maneno mapya yametungwa kwenye makala. Kigezo kinaorodhesha maneno mapya na Kiingereza yao, na pia kinaweka makala kwenye jamii ya 'kurasa zinazo maneno yaliyotungwa mapya'. Watu wengine wanapata nafasi ya kutazama maneno mapya. Neno likipatikana kwenye kamusi fulani au kama baadaye, neno lingine linatungwa nje ya Wikipedia, basi, neno la Wikipedia linaweza kufutwa na lingine kuwekwa badala yake. Tunao pia nia ya kuorodhesha majina haya mapya yote kwenye ukurasa ya pekee ya 'Maneno yaliyotungwa kwenye Wikipedia' ila hatujafanya bado - kuna mambo mengi ya kufanya!

Je, mnaonaje? Lloffiwr (majadiliano) 17:54, 25 Oktoba 2009 (UTC)[jibu]

Wazo ni zuri. Kuna kigezo cha {{jaribio}} kinacholeta sanduku linalosema
"Makala hiyo kuhusu "JINA LA MAKALA" inatumia neno ambalo si kawaida na matumizi yake ni jaribio kwa jambo linalotajwa. Wasomaji wanaombwa kuchangia mawazo yao. Kamusi za Kiswahili ama zinatofautiana kuhusu matumizi ya neno hili au hazieleweki au hazina neno kwa jambo linalojadiliwa."
Unaonaje?
Menginevyo ukiwa Mwelisi nakuomba angalia makala za Uingereza, Britania, funguvisiwa ya Britania, Ufalme wa Muungano. Nilizianzisha nilipoona a)kweli Kiswahili hutumia "Uingereza" kama neno la pekee lakini b) niliona haja ya kuwa na neno kwa "Britain" maana nilishindwa kusema namna gani kuhusu uhusiano wa Uingereza, Welisi na Uskoti ndani ya - nini? Uingereza tena???. Hapa niliamua kutumia neno lisilo kawaida "Britania" (labda nimeiunda?) kwa matumaini ya kamba litaeleweka ila tu sijaendelea na makala hizi wakati ule nilitaka kusubiri - basi iebaki vile. --Kipala (majadiliano) 04:58, 26 Oktoba 2009 (UTC)[jibu]
Nimeingiza sentensi moja kwenye makala ya Uingereza. Sijui kama inasaidia kitu? Matumizi ya maneno haya yana siasa, tena kali! Lloffiwr (majadiliano) 16:54, 7 Novemba 2009 (UTC)[jibu]
Nawapongeza kwa hatua muhimu. Asanteni! Upande wa jamii ya {{jaribio}} naona shida kwamba sanduku halitaji ni neno lipi lisilo la kawaida. Kwa mfano, makala ya Ujerumani ipo katika jamii ya jaribio lakini siyo rahisi kugundua istilahi yenye mashaka humo. Naomba tupate orodha ilivyoelezwa na Bw.Lloffiwr hapo juu. Tusonge mbele! --Baba Tabita (majadiliano) 10:16, 26 Oktoba 2009 (UTC)[jibu]
Kiasi ni kweli Baba Tabita anachosema juu ya jamii ya {{jaribio}}. Je yuko anayejua njia ya kuingiza neno husika ndani ya sanduku lile la kigezo likionekana? Njia nyingine ya kutumia kigezo hiki ni kubadilisha maneno yake kidogo ili kutaja jina la makala tu (hii inaonyeshwa ndani yake!). Je hii inaweza kusaidia?
Mfano: Makala ya "Britania" linatumia neno la jaribio. Kama neno la jaribio ni sawa na jina la makala tunajua jinsi gani kuionyesha ndani ya sanduku; ni jambo tu kusahihisha maneno ya sanduku. Kwa mfano: "{{PAGENAME}}" ni neno ambalo si kawaida na matumizi yake ni jaribio kwa jambo linalotajwa..." "PAGENAME" katika mabano haya huonyesha jina la makala. Inasaidia kwa makala kama "Britania" lakini haiwezi kutumiwa kwa makala kama "Ujerumani" ambako neno lisilo kawaida liko ndani ya makala (ama Alpi au Dola Takatifu...) na hapa nakubali na Oliver haisaidii kitu kama haitajwi. --Kipala (majadiliano) 19:40, 26 Oktoba 2009 (UTC)[jibu]
Niko tayari kutengeneza kigezo chenyewe kwa kuongeza kigezo cha jaribio, kwa kutumia mfano wa kigezo cha Kiwelisi. Maneno yenyewe na Kiingereza (au lugha nyingine) chao yataandikwa ndani ya kigezo kitakapoingizwa kwenye makala. Kwa mfano katika makala ya Ujerumani pataandikwa kitu kama {{jaribio| lugha_ya_asili = Kijerumani | maneno_ya_jaribio = Alpi, Dola Takatifu | maneno_ya_asili = Alpen, Heiliges Römisches Reich}} na lugha ya asili na maneno ya jaribio na ya asili yataonekana ndani ya kigezo. Ila tu sitaweza kukamilisha haraka - nina mambo mengi ya kufanya hapa na huku. Salaam za kutoka Welisi. Lloffiwr (majadiliano) 21:48, 26 Oktoba 2009 (UTC)[jibu]
Naomba uonyeshe kiungo kwenda kigezo kile cha Kiwelisi au popote nipate kuangalia yaliyomo yake.
Mpendwa Kipala - kiungo cha kwanza juu inaenda kwa kigezo cha Kiwelisi. Kiungo cha pili kinaenda kwa jamii ya kurasa zinazotumia kigezo - ukitaka kuona mfano bonyeza moja wa kurasa kwenye jamii. Kigezo cha Kiwelisi lazima ibadilishwe ili kuweza kuweka lugha yeyote iwe lugha ya asili. Kazi njema. Lloffiwr (majadiliano) 13:44, 27 Oktoba 2009 (UTC)[jibu]
Nimepanga kuongeza kigezo cha jaribio hapa. Je, inafaa? Kama itakubalika nitabadilisha kigezo cha sasa. Ikibadilishwa itabidi makala zinazotumia kigezo hiki tayari yaongezwa maneno ya asili, lugha ya asili na maneno ya jaribio. Lloffiwr (majadiliano) 20:49, 1 Novemba 2009 (UTC)[jibu]
Je, kuna maona juu ya mabadiliko niliyoyapendekeza? Labda badala ya kubadilisha kigezo cha Jaribio, ingekuwa rahisi zaidi kuandika kigezo kipya, labda Jaribio1, ili isibidi turekebishe viungo vyote vya Kigezo:Jaribio vilivyopo tayari? Lloffiwr (majadiliano) 13:57, 21 Novemba 2009 (UTC)[jibu]
Kimsingi naona kigezo jinsi unavyoiandaa kitu kizuri. Awali sijaandika bado maoni yangu kwa sababu nilishindwa namna ya kuitumia. Naomba kwa wajinga kama mimi (au watu ambao hawahariri vigezo kila siku) uongeze maelezo: je tunfanye nini ili neno lionekane?--Kipala (majadiliano) 15:26, 22 Novemba 2009 (UTC)[jibu]
Nakusikia Kipala. Ili mfano uonekana vizuri imebidi nitengeneze kigezo cha 'Jaribio1' moja kwa moja. Nimekiingiza kwenye makala ya Britania kama mfano. Kigezo kipo chini ya kigezo cha jaribio. Unaonaje? Lloffiwr (majadiliano) 21:18, 23 Novemba 2009 (UTC)[jibu]
Naona kwamba mada hii imesahauliwa kidogo, labda kwa sababu ya mashindano. Je, kuna maoni gani kuhusu mfano wa kigezo cha jaribio? Lloffiwr (majadiliano) 11:51, 27 Februari 2010 (UTC)[jibu]

Nimeandika mwongozo wa kutunga istilahi unao eleza matumizi ya kigezo hiki. Kama haieleweki, tafadhali mniaeleze namna ya kuiboresha. Pia nimetengeneza orodha ya istilahi mpya. Je, inafaa? Lloffiwr (majadiliano) 16:51, 25 Julai 2010 (UTC)[jibu]

Kurekebisha jumbe[hariri chanzo]

Riccardio Riccioni amesema kwenye sehemu ya Istilahi ya wikipedia: 'Pamoja na hayo, bado kuna makosa ya wazi, kwa mfano: ukarasa, masahihisho zangu, n.k.'. Ni kweli. Kuna kazi inayofanyika translatewiki.net ya kutafsiri jumbe. Ingekuwa vizuri kupata wafasiri wengine pale. Lakini kuna kazi pia ya kufuta jumbe zingine zilizopitwa na wakati hapa Wikipedia ya Kiswahili. Mkitazama orodha ya jumbe mtaona kwamba kuna jumbe zingine ambazo zimeshasahihishwa kule translatewiki.net lakini ujumbe wa zamani ndiyo ule unaoonekana hapa Wikipedia, kwa mfano ujumbe wa 'printableversion'. Unaotakiwa ni kufuta ujumbe uliopo hapa, ikiwa ujumbe wa kutoka translatewiki.net unafaa zaidi. Ni wakabidhi tu ambao wanaweza kusahihisha au kufuta jumbe. Kwa hiyo naomba wakabidhi waangalie jumbe na wazifute jumbe zingine au wazisahihishe. Lloffiwr (majadiliano) 14:12, 7 Novemba 2009 (UTC)[jibu]

Kiswahili Wikipedia Challenge[hariri chanzo]

Google has announced a Kiswahili Wikipedia Challenge, to run from November 25, 2009, to January 15, 2010. Contest is open to residents of Kenya and Tanzania. --LA2 (majadiliano) 21:10, 12 Novemba 2009 (UTC)[jibu]

Now one would like to speak your language fluently... However I think this is a great thing for the Kiswahili Wikipedia! Like your language by the way. Tanzania - in Swedish 09:57, 13 Novemba 2009 (UTC)[jibu]
Yeah! We've already alerted about the Challenge and some of us from the community are going to be the reviewers to the articles which are going to be created by those who are participating into the challenge! Thanks for the notice, though we've already know! Cheers.--Muddyb MwanaharakatiLonga 10:11, 13 Novemba 2009 (UTC)[jibu]
I'm working on instructions for the students who sign up. Maybe they should all post a greeting message here on the Jumuia? Sj (majadiliano) 23:04, 20 Novemba 2009 (UTC)[jibu]
If that would be easy for them, then let them post their greeting message at here!--Muddyb MwanaharakatiLonga 06:41, 21 Novemba 2009 (UTC)[jibu]

I'm a participant in the Swahili Wikipedia challenge, I felt I might have been awarded points unfairly. Can I please have my articles looked at afresh.[[1]] [2]

IP limit for new account creation[hariri chanzo]

We have ~800 potential editors signed up to take part in the challenge (!!) you can see ~100 of them have signed up over the past week. Most of the universities or computer labs involved share an IP address, however, and so can't all create accounts at once. We can request that this limit be raised. (However raising it too high imposes a vandalism risk for all wikis, because of unified login.)


Pendekezo: Jinsi ilivyo sasa, kila anwani ya IP inaweza kusajili akaunti 6 kila siku si zaidi. Kutokana na mashindano ya kuandika makala, wiki hii iongeze idadi ya akaunti zinazoweza kusajiliwa kwa kila anwani ya IP iwe 100 kila siku kwa kipindi cha wiki mbili zijazo.
Proposal: Currently, there is a limit of 6 new accounts per day per IP address. For KWC, this wiki should raise the limit on new account creation per IP to 100/day for the next two weeks.

Unga mkono/Support

Pinga/Oppose

Great start... now linked from Mwanzo as mtu anaweza kuihariri. Sj (majadiliano) 23:23, 3 Desemba 2009 (UTC)[jibu]

Baada ya Muddy kuanza nimemaliza kazi; 1) Nimehamisha makala sasa inaitwa "mwongozo" (tazama majidiliano kwenye ukurasa huu); 2) "Fungasha" nimeweka tu kielekezo kwenye ukurasa wa Kiingereza maana hatuna kurasa hizi. 3) Naomba wengine waangalie na kuchangia! --Kipala (majadiliano) 11:49, 6 Desemba 2009 (UTC)[jibu]

Tafsiri ya "unranked"[hariri chanzo]

Nimeongezea Kigezo:Uainishaji (Mimea) makundi ambayo ni "unranked". Katika uainisho wa mimea wa kisasa kuna makundi ("clades") ambayo hayajawepa hadhi rasmi. Yanaitwa "unranked taxa". Nimetafsiri "unranked" kwenye bila tabaka lakini sina hakika. Mnaonaje? Pia, nani atapendekeza tafsiri ya "taxon"? ChriKo (majadiliano) 22:33, 5 Desemba 2009 (UTC)[jibu]

Je vipi "ngazi bila tabaka"? Halafu ombi: Kwa Kigezo cha namna hii ni vema kama ukurasa unaonyesha pia yaliyomo yake mfano Kigezo:Mto. Asante kwa kazi! --Kipala (majadiliano) 11:55, 6 Desemba 2009 (UTC)[jibu]
KWC Mtumiaji huyu ni mshiriki katika Shindano la Wikipedia ya Kiswahili la 2009.   (Submissions)
(for individuals)