Ludwig van Beethoven

Kutoka Wikipedia, kamusi elezo huru
Rukia: urambazaji, tafuta
Ludwig van Beethoven (1770–1827); picha ya Joseph Karl Stieler, 1820

Ludwig van Beethoven (16 Desemba 1770 - 26 Machi 1827) alikuwa mtungaji wa muziki na mpiga piano kutoka nchi ya Ujerumani.

Alizaliwa mjini Bonn akiwa mtoto wa mwanamuziki aliyemfundisha kinanda tangu utoto. 1787 akiwa kijana alisafiri Vienna iliyokuwa mji mkuu wa Dola Takatifu la Kiroma kwa matumaini ya kukutana na Wolfgang Amadeus Mozart akarudi 1792 alipopata mafunzo kuoka Joseph Haydn. Tangu 1793 alikuwa maarufu mjini Vienna kama mpiga kinanda akaendelea kutunga muziki yake. Alipata usaidizi na wateja kati ya makabaila wa makao makuu ya Kaisari.

Tangu miaka ya 1796 alianza kupoteza uwezo wake wa kusikia wake akaendelea kuwa kiziwi lakini aliamua kuendelea na muziki yake. Kuna hadithi ya kwamba alioongoza simfonia ya tisa na mwishowe watu walimgeuza aangalie wasikilizaji kwa sababu hakusikia jinsi walivyopiga makofi.

Aliweza kuendelea kutunga na kuongoza musiki na kupiga piano. Alifunga fimbo kwenye kinanda akaishika kwa meno na kusikia tetemeko la piano kupitia fimbo na meno yake.

Aliaga dunia alipokuwa na umri wa miaka 57.


DBP - 200 Jahre Beethoven - 10 Pfennig - 1970.jpg


Orodha ya Wanamuziki wa kipindi cha Romatiki
Alkan Balakirev Beethoven Bellini Berlioz Berwald Bizet Borodin Brahms Bruckner Chopin Cui Dvořák Elgar Field Franck Glinka Grieg Liszt Mahler Mendelssohn Mussorgsky Rachmaninoff Rimsky-Korsakov Saint-Saëns Schubert Schumann Smetana Strauss Tchaikovsky Verdi Wagner Wolf Weber
Musical notes.svg Makala hii kuhusu mwanamuziki fulani wa Ulaya bado ni mbegu.
Je, unajua kitu kuhusu Ludwig van Beethoven kama wasifu wake, habari za maisha au kazi yake?
Labda unaona habari katika Wikipedia ya Kiingereza au lugha nyingine zinazofaa kutafsiriwa?
Basi unaweza kuisaidia Wikipedia kwa kuihariri na kuongeza habari.