Richard Strauss
Richard Strauss (alizaliwa mjini Munich tar. 11 Juni 1864 na kufariki mjini Garmisch-Partenkirchen, Bavaria, 8 Septemba 1949) alikuwa mtunzi wa Opera na mwelekezi mashuhuri kutoka nchini Ujerumani. Huyu alipata bahati ya kuwa mashuhuri tangu yungali bwana mdogo na toni zake zilitumika katika mabendi mbalimbali katika Ulaya nzima.
Baada ya 1900 alitumia muda wake mwingi kwa kutunga opera. Moja kati ya opera zake zilizowahi kuwa maarufu ni "Der Rosenkavalier", aliitunga kunako mwaka wa 1910, na ilitamba saana.
Strauss alikuwa moja kati ya watunzi wakubwa wa mwisho kutunga muziki kwa mtindo wa Romantic. Alipenda sana muziki wa Wagner ambaye alipata athari kubwa za muziki wake, lakini pia alipenda na ule wa Mozart na kazi zake nyingi zaonyesha kuwa na ufaa mkubwa kama vile zilivyokuwa zile za muziki wa Mozart. Strauss alikuwa mwelekezi mzuri sana na mara nyingi aliekeza miziki yake mwenyewe.
Viungo vya nje
[hariri | hariri chanzo]- Chronological list of Strauss's works Archived 25 Agosti 2006 at the Wayback Machine.
- Richard Strauss online Archived 27 Aprili 2009 at the Wayback Machine.
- Public Domain Sheet Music of Richard Strauss at IMSLP
- Shughuli au kuhusu Richard Strauss katika maktaba ya WorldCat catalog
- Timeline biography of Strauss at Richard-Strauss.com
- Shughuli au kuhusu Richard Strauss katika maktaba ya WorldCat catalog