Wikipedia:Kutunga istilahi
Mara nyingine makala inazungumza mambo yanayohitaji istilahi ambaye haijatungwa katika Kiswahili, au kamusi zimetunga tofauti tofauti. Ikiwa istilahi inatungwa hapa katika Wikipedia ya Kiswahili ni vyema kuweka kisanduku katika makala, ili kueleza kwamba makala inayo maneno mapya. Hii itarahisisha majadiliano ya maneno mapya. Kisanduku kinawekwa kwa kutumia kigezo. Pia ni vyema kuongeza neno katika orodha ya istilahi mpya, ili wasomaji waweze kupata kuelewa maana ya neno jipya fulani. Halafu, istilahi nyingine ikipatikana baadaye, nje ya Wikipedia, tutaweza kutoa neno lililotungwa hapa, neno lingine lichukue nafasi yake.
Kigezo cha jaribio1
[hariri chanzo]Kisanduku cha kuarifu kwamba istilahi iliyotungwa inatumiwa katika makala kinawekwa kwa kutumia kigezo cha "Jaribio1".
Mfano: ukiandika
{{Jaribio1|maneno_ya_asili = Alpen, Heiliges Römisches Reich|lugha = Kijerumani|maneno_ya_jaribio = Alpi, Dola Takatifu}}
utapata kisanduku hiki
Kigezo kinafaa kuwekwa mwishoni mwa ukurasa, kama kilichowekwa katika mfano wa makala ya Britania.