Nenda kwa yaliyomo

Wikipedia:Istilahi za wiki

Kutoka Wikipedia, kamusi elezo huru
Jamii (Category)
Jamii ni mkusanyiko wa makala zote zinazohusika na kichwa fulani, pamoja na vijamii vyake; kwa mfano Jamii:Nchi za Afrika. Majina ya jamii zote ambazo ukurasa umewekewa ndani zao yameandikwa mwishoni mwa ukurasa. Kichwa cha jamii zote ni Jamii:Jamii Kuu. Unaweza kutafuta jamii fulani kwa kuingiza Jamii:jina linalotafutwa ndani ya sanduku la kutafuta.
Maelezo mengine yanapatikana hapa.
Kijamii (Subcategory)
Kuna jamii moja tu, Jamii:Jamii Kuu, ambaye si sehemu ya jamii nyingine. Jamii zote zinazoonekana kwenye orodha ya vijamii kwenye ukurasa wa jamii nyingine ni vijamii vyake.
Mkabidhi (Admin, sysop)
Mkabidhi ni mtumiaji anayepewa majukumu kadhaa ya kutunza wiki. Anaweza kufuta kurasa, kulinda kurasa na kuzuia watumiaji wanaofanya fujo. Wezo za wakabidhi zinaelezwa katika "Wezo za kundi za watumiaji".
Mtumiaji (User)
Mtu anayeandika katika wiki hii au anayefanya kitu chochote katika wiki. Wakati mwyingine mtumiaji anaitwa mhariri. Wezo za watumiaji zinaelezwa katika "Wezo za kundi za watumiaji".