Nenda kwa yaliyomo

Milki ya Mali

Kutoka Wikipedia, kamusi elezo huru
(Elekezwa kutoka Ufalme wa Mali)

Kuhusu nchi ya kisasa angalia Mali

Eneo la Dola la Mali.

Milki ya Mali ilianza kama ufalme mdogo wa Wamalinke kando ya Dola la Ghana.

Wakati wa karne ya 13 ilianza kupanuka chini ya mfalme Sundiata Keita. Sundiata mwenyewe alipokea Uislamu mnamo 1240 BK na wafalme baada yake waliendela kuwa Waislamu.

Mfalme wa Mali aliyejulikana zaidi ndiye Mansa Kankan Musa I (13121337). Miaka 1324-1325 alihiji kwenda Makka. Alisafiri na dhahabu nyingi sana. Huku Misri alitoa zawadi kiasi cha kuharibu thamani ya dhahabu kwa miaka 12 iliyofuata.

Wakati ule eneo liliweza kuwa la kilometa mraba 1,300,000 na wakazi milioni 20; mji wa Timbuktu ulikuwa kitovu cha biashara na elimu iliyojulikana kote katika umma wa Kiislamu hata Ulaya.

Katika karne ya 14 BK uwezo na utawala wa Mali ulipungua na Dola la Songhai lilichukua nafasi yake.

Makala hii kuhusu mambo ya kihistoria bado ni mbegu.
Je, unajua kitu kuhusu Milki ya Mali kama enzi zake au matokeo yake?
Labda unaona habari katika Wikipedia ya Kiingereza au lugha nyingine zinazofaa kutafsiriwa?
Basi unaweza kuisaidia Wikipedia kwa kuihariri na kuongeza habari.