Pizza

Kutoka Wikipedia, kamusi elezo huru
Rukia: urambazaji, tafuta
Pizza "Margerita" ni namna asilia ya pizza kutoka Napoli
Pizza ya pepperoni (=pilipili)
Pizza kubwa namna hii inakatwa vipande
Pizza inavyookwa katika jiko

Pizza (matamshi ya Kiitalia pid-za) ni chakula chenye asili nchini Italia kilichosambaa kote duniani. Ni kipande cha mkate bapa kinachofunikwa kwa mchuzi mnene wa nyanya na vipande vya jibini. Mara nyingi vipande vyembamba vya mboga mbalimbali, nyama au samaki vinaongezwa pamoja na jibini. Yote huokwa katika joko, jibini inayeyuka na kuunganisha sehemu nyingine za pizza.

Historia ya pizza[hariri | hariri chanzo]

Mtangulizi wa pizza na pia chanzo cha jina ni "pita" ya Kigiriki. Tangu milenia watu wa nchi za Mediteranea walitengeneza chakula cha moto kwa kuoka mkate bapa pamoja na majani, mafuta na jibini, pia nyama iliyosagwa. Hii "pita" ya Wagiriki inapatikana pia katika nchi jirano kwa mfano Uturuki kwa jina "pide".

Pizza yenyewe ina chanzo chake katika mji wa Napoli (Italia kusini) wakati wa karne ya 19. Mwanzoni pizza ilisambaa kutoka Napoli kwa sehemu nyingine Italia. Baadaye wahamiaji kutoka Italia walileta pizza hadi nchi walipohamia na hapo wenyeji wa nchi hizi walianza kupenda chakula hiki.

Hatua nyingine za usambazaji ilikuwa utengezaji wake viwandani ambako pizza zinaandaliwa na kugandishwa katika chumba cha barafu. Kama chakula barafu huuzwa kupitia maduka penye friza na kuokwa katika joko la nyumbani. Kutokana na uwingi wa ladha na urahisi wa kuiweka mezani pizza barafu namna hizi za pizza zinauzwa kwa wingi katika mazingira penye maduka ya friza.

Nanma ya kutegeneza pizza[hariri | hariri chanzo]

Kinyunga kinatenegezwa kwa kutumia unga wa ngano, maji, chumvi, hamira na mafuta kidogo. Kinyunga kinakaa kwa muda wa angalau saa 1 halafu kinatandikwa nyembamba sana. Hapa ndipo tofauti muhimu na aina za "pita". Kinyunga bapa hufunikwa ama kwa vipande vyembamba vya nyanya au mchuzi mnene wa nyanya uliopikwa pamoja na viungo kama vitunguu saumu na majani yenye ladha; nyanya hufunikwa kwa jibini iliyosagwa au iliyokatwa bapa nyembamba sana. Hapo ndipo pizza asilia inayowekwa katika joko na kuokwa kwa joto kubwa iwezekanavyo mara nyingi sentigredi 400-500 kwa dakika chache tu.

Kuna namna nyingi kubadilisha na kuongeza ladha ya pizza kwa kuongeza viungo vingine juu na ndani ya kanda la jibini. Mara nyingi vipande vyembamba vya nyama kama soseji, samaki au wanyama wengine wa baharini, uyoga, mboga kama vitunguu, zeituni, pilipili, pilipili hoho na mengine vyatandikwa hapa. Hakuna vyakula visivyoweza kukatwa vyembamba na kutumiwa hapa.