Mkoa wa Unguja Kusini

Kutoka Wikipedia, kamusi elezo huru
Mkoa wa Kusini Unguja, Tanzania

Mkoa wa Unguja Kusini ni moja ya mikoa 26 za Tanzania kwenye kisiwa cha Unguja. Eneo la mkoa ni 854 km² likiwa na wakazi 94,504 (sensa 2002). Makao makuu yako Koani. Kuna wilaya mbili ikiwa Wilaya ya Kati ina wakazi 62,537 na Wilaya ya Kusini ina wakazi 31,967.

Wakazi wa eneo hili la kisiwa cha Unguja mbali na kujishughulisha na shughuli za uvuvi kwenye Bahari ya Hindi, wakazi wa Kusini Unguja ni maarufu pia kwa kilimo cha zao la karafuu, zao linalokifanya Kisiwa cha Zanzibar kujulikana zaidi kama kisiwa cha viungo.

Makala hii kuhusu maeneo ya Unguja bado ni mbegu.
Je unajua kitu kuhusu Mkoa wa Unguja Kusini kama historia yake, biashara, taasisi zilizopo, watu au utamaduni?
Labda unaona habari katika wikipedia ya Kiingereza au lugha nyingine zinazofaa kutafsiriwa?
Basi unaweza kuisaidia Wikipedia kwa kuihariri na kuongeza habari.
Tafadhali usiingize majina ya maafisa au viongozi wa sasa maana wanabadilika mno.