Kaisarea Baharini
32°30′0″N 34°53′30″E / 32.50000°N 34.89167°E
Kaisarea Baharini (kwa Kigiriki Παράλιος Καισάρεια, Parálios Kaisáreia) ulikuwa mji wa Palestina kuanzia mwaka 10 KK hadi 1265 BK.
Kwa sasa ni sehemu ya Hifadhi ya Taifa la Israeli katika bonde la Sharon[1].
Ulianzishwa na mfalme Herode Mkuu ukawa makao ya liwali wa Dola la Roma aliyetawala Palestina.
Baadaye ukawa kituo muhimu cha Ukristo, ambapo Mtume Petro alibatiza akida Korneli na familia yake (Mdo 10:1-11:18).
Ndipo alipoishi Filipo mwinjilisti (Mdo 8:40) ambaye alimkaribisha Mtume Paulo kwa siku kadhaa (Mdo 21:8-10) katika moja ya nafasi yake ya kupitia mjini huko (Mdo 9:30; 18:22).
Baadaye Paulo alikaa gerezani huko kwa zaidi ya miaka miwili akisubiri kuhukumiwa, mpaka alipokata rufaa kwa Kaisari Nero (23:23; 15:1-13).
Tanbihi
[hariri | hariri chanzo]- ↑ "Caesarea National Park". Ilihifadhiwa kwenye nyaraka kutoka chanzo mnamo 2017-10-26. Iliwekwa mnamo 2017-10-21.
Marejeo
[hariri | hariri chanzo]- Joseph Patrich, "Caesarea in the Time of Eusebius" in S. Inowlocki, C. Zemagni (eds.), Reconsidering Eusebius: Collected papers on literary, historical, and theological issues (2011), 1–24.
- Lehmann, Clayton Miles; Holum, Kenneth G. (2002). The Greek and Latin Inscriptions of Caesarea Maritima. University of Michigan. ISBN 0897570286.
- Raban, Avner; Holum, Kenneth G. (1996). Caesarea Maritima: a retrospective after two millennia. Leiden: Brill. ISBN 90-04-10378-3.
Viungo vya nje
[hariri | hariri chanzo]- Jewish Encyclopedia: Cæsarea by the Sea
- PBS Frontline – Caesarea Maritima
- Archaeology of Caesarea
- Photo gallery of Caesarea Maritima
- Photo gallery of Caesarea Maritima
- Gavriel Solomon, Caesarea National Park: Conservation Maintenance, Israel Antiquities Authority Site - Conservation Department
Makala hii kuhusu maeneo ya Asia bado ni mbegu. Je unajua kitu kuhusu Kaisarea Baharini kama historia yake, biashara, taasisi zilizopo, watu au utamaduni? Labda unaona habari katika wikipedia ya Kiingereza au lugha nyingine zinazofaa kutafsiriwa? Basi unaweza kuisaidia Wikipedia kwa kuihariri na kuongeza habari. |