Filipo mwinjilisti
Filipo mwinjilisti ni Myahudi wa karne ya 1 anayejulikana hasa kutokana na Matendo ya Mitume.
Anaheshimiwa na madhehebu mbalimbali ya Ukristo kama mtakatifu.
Sikukuu yake huadhimishwa na Kanisa Katoliki na Anglikana tarehe 11 Oktoba[1][2], kumbe katika Makanisa ya Kiorthodoksi ni tarehe 6 Juni.
Katika Biblia
[hariri | hariri chanzo]Alikuwa mmojawapo kati ya wanaume saba wa lugha ya Kigiriki katika Kanisa mama la Yerusalemu waliochaguliwa kushughulikia mafukara kwa niaba ya Mitume wa Yesu (Mdo 6).
Baadaye alijitokeza kama mhubiri na mtendamiujiza huko Samaria, alipoongoa na kubatiza wengi kati ya wakazi, bila kujali uadui wa jadi kati yao na Wayahudi (Mdo 8).
Baadaye aliongozwa na Mungu kuongozana na towashi muhimu wa Ethiopia akambatiza karibu na Gaza (Mdo 8).
Baadaye tena alikuwa akiishi Kaisarea Maritima, pamoja na mabinti wake wanne ambao walikuwa mabikira na manabii, Mtume Paulo alipopitia huko mwaka 58 akielekea Yerusalemu (Mdo 21)[3].
Katika mapokeo
[hariri | hariri chanzo]Mapema alianza kuchanganywa na Mtume Filipo, pia kwa sababu ya utume mkubwa alioufanya.[4]
Mapokeo ya baadaye yanasimulia kwamba alikuwa askofu wa Trale katika Uturuki wa leo.
Tazama pia
[hariri | hariri chanzo]- Watakatifu wa Agano la Kale
- Orodha ya Watakatifu Wakristo
- Orodha ya Watakatifu wa Afrika
- Orodha ya Watakatifu Wafransisko
Tanbihi
[hariri | hariri chanzo]- ↑ "Martyrologium Romanum", Typis Vaticanis, Editio Altera, 2004, entry for 11 October
- ↑ Calendar of saints (Episcopal Church in the United States of America)
- ↑ https://www.santiebeati.it/dettaglio/91612
- ↑ see further George Salmon, Introduction to the New Testament, 7th ed., p. 313 sqq.
Viungo vya nje
[hariri | hariri chanzo]- Apostle Philip the Deacon of the Seventy Orthodox icon and synaxarion
- Who is St. Philip the Evangelist Ilihifadhiwa 23 Novemba 2009 kwenye Wayback Machine.
- IVP New Testament Commentary on Philip in Acts 8 Ilihifadhiwa 19 Mei 2014 kwenye Wayback Machine.
Makala hii kuhusu mtu wa Biblia bado ni mbegu. Je, unajua kitu kuhusu Filipo mwinjilisti kama habari za maisha au kazi yake? Labda unaona habari katika Wikipedia ya Kiingereza au lugha nyingine zinazofaa kutafsiriwa? Basi unaweza kuisaidia Wikipedia kwa kuihariri na kuongeza habari. |